News-Details

News >Details

MZUMBE NA IORA KUIBUA FURSA ZA KIUCHUMI, UHIFADHI RASILIMALI BAHARI

MZUMBE NA IORA KUIBUA FURSA ZA KIUCHUMI, UHIFADHI RASILIMALI BAHARI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis ameitaka jamii kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kutunza na kuhifadhi mazingira ili kuwa na kizazi chenye uelewa na kuthamini mazingira hususan uchumi wa bluu. Ameyasema hayo leo tarehe 22/10/2024 wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya Kimataifa wa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Hotel Seascape, Dar es salaam iliyoratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe, Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kushirikisha nchi ambazo zimezunguka Ukanda wa bahari ya Hindi Naibu Waziri Khamis, ametoa rai kwa wadau wote wa ukanda wa bahari ya Hindi (IORA), kuhakikisha kwamba jamii inapata uelewa na elimu sahihi ya kuhusu utunzaji wa Mazingira. “Sisi wasomi twendeni tukatoe elimu kwa jamii kuhusu kutunza Mazingira, jamii yetu haina uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Ikolojia, kaboni na namna bora ya utunzaji wa mazingira twende tukawaelimishe watu jinsi ya kuvuna kaboni” alisisitiza Mhe Khamis. Amesema uelewa wa masuala ya Kaboni na matumizi sahihi ya rasilimali za bahari kupitia uchumi wa bluu ni muhimu kwa jamii inayozunguka mazingira ya pwani kwa kuwa husaidia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa rai kwa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) kuweka nguvu zaidi katika kutoa elimu ya matumizi endelevu ya rasilimali za bahari. “Tunaomba mtusaidie kuelimisha jamii ili kutunza Mazingira.”Alisitiza Mhe Khamis Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema wakati ni sasa wa kuunganisha nguvu za wasomi, watafiti na wanamazingira kuendelea kuhimiza uhifadhi wa mazingira na kusisitiza matumizi sahihi ya uchumi wa bluu kama njia ya kulinda mazingira na chanzo cha maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho. "Nchi au ukanda unaohusishwa na IORA (Indian Ocean Rim Association umeanza kugundua na kutumia faida za uchumi wa buluu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa njia endelevu. Alifafanua Prof.Mwegoha.

None
None
None
None