News-Details

News >Details

UBALOZI WA INDIA WATEMBELEA CHUO KIKUU MZUMBE KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIELIMU

UBALOZI WA INDIA WATEMBELEA CHUO KIKUU MZUMBE KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIELIMU

Chuo Kikuu Mzumbe kimepokea ugeni kutoka Ubalozi wa India nchini Tanzania tarehe 26 Mei 2025, katika ziara iliyoongozwa na Mkuu wa Utawala, Katibu wa pili anayeshughulikia ITEC, Elimu na Afya kutoka Ubalozi wa India, Bw. Rajnish Kumar akiambatana na Msaidizi wa Usalama kutoka Ubalozi wa India, Bw. Godse Nanaso. Ugeni huo ulipokelewa rasmi na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Orest Masue ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada ya Awali akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kimataifaji na Baraza la Wahitimu, Dkt. Lucy Massoi. Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Serikali ya India, kwa kuangazia maeneo muhimu kama vile: Fursa za ufadhili wa masomo kupitia programu za ICCR (Baraza la Mahusiano ya Kitamaduni la India) na ITEC (Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi wa India). Ushirikiano mpana katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kubadilishana wanafunzi na wahadhiri, kufanya tafiti za pamoja, na matumizi ya teknolojia ya kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji. Kupitia ziara hii, Chuo Kikuu Mzumbe na Ubalozi wa India wamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa muda mrefu katika kuinua ubora wa elimu ya juu nchini Tanzania.

None
None
None
None
None
None
None
None