News-Details

News >Details

DKT. SHEIN APOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA CHUO KIKUU MZUMBE

DKT. SHEIN APOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA CHUO KIKUU MZUMBE

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amepokea taarifa ya maendeleo ya Chuo iliyowasilishwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha leo tarehe 06 Novemba, 2024 Zanzibar. Katika kuwasilisha taarifa hiyo ya maendeleo kwa kipindi cha miezi mitatu (Agosti hadi Oktoba 2024), uongozi wa Chuo umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Saida Yahya – Othman, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri) Prof. Eliza Mwakasangula. Taarifa hiyo iliyowasilishwa mapema leo imejikita kueleza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe, ikiwa ni pamoja na taarifa za utekelezaji wa miradi ya Chuo kwa fedha za ndani, hali na ustawi wa Watumishi na Wanafunzi, kujenga uwezo wa watumishi wa Chuo, kuimarisha ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kusaini hati za makubaliano ya ushirikiano na mashirika, Taasisi na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi. Aidha kupitia taarifa hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo ameeleza juu ya miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa na Chuo kwa ufadhili wa Serikali, akiutaja mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) na kueleza namna ambayo Chuo Kinaendelea kunufaika kupitia mradi huo pamoja na matarajio yake huku akieleza nia ya dhati ya uongozi wa Chuo katika kuendelea kusimamia kwa weledi hatua za utekelezaji wa mradi huo. Vilevile, Makamu Mkuu wa Chuo ameeleza hatua za maandalizi ya Mahafali ya 23 na kwamba baraza la chuo na menejimenti wanaendelea kufuatilia hatua za maandalizi ili kuleta ufanisi wa mahafali hayo. Akizungumza na viongozi hao, Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein ameeleza namna alivyofurahishwa na jitihada zinazofanywa na Chuo hasa katika utekelezaji wa miradi, kuanzisha ushirikiano na taasisi nyingine pamoja kutambua na kuthamini hali za wafanyakazi kwa kuwapandisha vyeo wale wote wanaostahili. Aidha, amewataka viongozi wa Chuo kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Chuo.

None
None
None