News-Details

News >Details

MAKAMU MKUU WA CHUO AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA NDAKI YA DAR ES SALAAM

MAKAMU MKUU WA CHUO AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA NDAKI YA DAR ES SALAAM

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amefanya ziara ya kikazi Ndaki ya Dar es Salaam tarehe 9 Juni 2025 na kuzungumza na wanafunzi katika kikao kilicholenga kukagua maendeleo yao, kusikiliza changamoto, maoni, pamoja na kutoa dira ya uongozi wa chuo kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa ustawi wa elimu na maisha ya wanafunzi chuoni hapo. Katika kikao hicho, Prof. Mwegoha amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwa na uzalendo kwa Chuo na kwa kulinda jina lake, kuwajibika, na kuishi tunu za Chuo Kikuu Mzumbe. Amesisitiza kuwa kila mwanafunzi anapaswa kulinda taswira ya chuo kwa kuwa inahusiana moja kwa moja na hadhi yao binafsi baada ya kuhitimu. Aidha, Prof. Mwegoha amehimiza wanafunzi kuzingatia usalama wao binafsi na mali za chuo, kujenga nidhamu ya kazi, na kutumia muda wao vizuri ili kujijenga kielimu na kiuzoefu. Aliongeza kuwa ni muhimu wanafunzi kuwa na ujuzi wa ziada nje ya masomo ya darasani (extra-curricular skills) kama vile mawasiliano, uongozi, na matumizi ya teknolojia, kwani ujuzi huo ni msaada mkubwa katika soko la ajira kwa sasa. Kwa nafasi yake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Hawa Tundui, amewasisitiza wanafunzi kuhusu wajibu wao wa kufuata miongozo ya Chuo Kikuu Mzumbe ili kufanikisha safari yao ya kitaaluma. Amesisitiza kuwa nidhamu, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) ni nguzo muhimu za mafanikio ya mwanafunzi wa kisasa. Amesema kuwa chuo kimeanzisha Kituo cha Ubora katika Ujifunzaji na Ufundishaji wa Kibunifu ambacho kitachangia kuboresha upatikanaji wa maudhu ya kitaaluma kwa njia ya kimtandao, hatua inayolenga kuboresha zaidi mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wote. Wanafunzi walitumia kikao hicho kuipongeza menejimenti ya chuo kwa juhudi kubwa zinazofanyika katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuishi, huku wakitoa mapendekezo ya kuimarisha zaidi huduma mbalimbali kama TEHAMA na huduma za maktaba.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None