News-Details

News >Details

KAMATI YA UADILIFU NA USULUHISHI WA MALALAMIKO HEET YAKAGUA MIRADI YA UJENZI MOROGORO NA TANGA

KAMATI YA UADILIFU NA USULUHISHI WA MALALAMIKO HEET YAKAGUA MIRADI YA UJENZI MOROGORO NA TANGA

Wajumbe wa Kamati ya Ushughulikiaji wa Malalamiko na Uadilifu katika Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Dkt. Hanifa Massawe, wamefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Jengo la TEHAMA katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe, eneo la Maekani, Morogoro tarehe 20 Juni 2025, pamoja na ujenzi wa Kampasi mpya ya Tanga, uliofanyika tarehe 24 Juni 2025 katika Wilaya ya Mkinga jijini Tanga. Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kufuatilia kwa ukaribu uzingatiaji wa taratibu, miongozo na viwango vya kimazingira, kijamii, afya na usalama mahala pa kazi katika miradi hiyo muhimu ya maendeleo. Katika Kampasi Kuu ya Chuo eneo la Maekani, Kamati ilifahamishwa kuwa ujenzi wa Jengo la Taaluma umefikia asilimia 57 na Jengo la TEHAMA umefikia asilimia 49, hatua inayodhihirisha maendeleo thabiti ya utekelezaji wa mradi huo unaolenga kuboresha miundombinu ya utoaji elimu ya juu nchini. Aidha, katika Kampasi ya Tanga, Kamati ilipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa majengo mbalimbali ambapo ujenzi wa Hosteli umefikia asilimia 51, Cafeteria asilimia 53, Jengo la Huduma za Afya asilimia 53, Nyumba za Watumishi asilimia 60, na Jengo la Taaluma asilimia 53. Katika ukaguzi huo, Kamati ilichambua vipengele kadhaa ikiwemo uzingatiaji wa sheria ya mazingira na usalama mahala pa kazi kama vile udhibiti wa vumbi, usimamizi wa taka kwa kutumia maeneo maalumu ya kuhifadhia, mifumo ya utenganishaji na urejelezaji wa taka, pamoja na matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira, kama vile matumizi ya taa za sola. Pia Kamati ilihakiki hali ya usafi, mpangilio wa vifaa na upatikanaji wa hewa ya kutosha katika maeneo ya kazi na maghala. Vilevile, Kamati ilitoa msisitizo kwa utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa kuhakikisha kuwa hakuna vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoripotiwa, pamoja na kuwepo kwa elimu ya usawa wa kijinsia na namna ya kuzuia vitendo hivyo kazini. Kamati ilihitimisha ziara yake kwa kutoa pongezi kwa timu za usimamizi wa miradi kwa juhudi wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa, kwa kuzingatia muda, thamani ya fedha, pamoja na usalama wa watu na mazingira.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None