News-Details

News >Details

KIKOSI KAZI MAALUMU CHAPONGEZWA KWA MAFANIKIO KATIKA UKUSANYAJI WA KODI YA PANGO SOKO LA USWAZI

KIKOSI KAZI MAALUMU CHAPONGEZWA KWA MAFANIKIO KATIKA UKUSANYAJI WA KODI YA PANGO SOKO LA USWAZI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, hii leo kwa niaba ya Menejimenti ya Chuo hicho amekabidhi zawadi za kumbukumbu pamoja na vyeti vya kutambua mchango wa watumishi waliokuwa sehemu ya Kikosi Kazi Maalumu cha ukusanyaji wa kodi ya pango katika Soko la Uswazi, lililopo Kampasi Kuu ya Chuo, Morogoro katika hafla iliyofanyika tarehe 25 Juni 2025, katika Ukumbi wa Mikutano, Maekani – Kampasi Kuu. Akizungumza katika tukio hilo, Prof. Mwegoha alieleza kuwa mchango wa kikosi kazi hicho maalumu umeleta mabadiliko chanya kwa taasisi, hususan katika kuongeza mapato na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masoko. “Tunatambua kwa dhati juhudi, uadilifu na kujitoa kwenu – mmefanya kazi kubwa ambayo imeleta matokeo ya kweli,” alisisitiza Prof. Mwegoha. Hatua hii ni kufuatia mpango wa Chuo Kikuu Mzumbe juu ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia Rasilimali na miradi inayomilikiwa na Chuo.

None
None
None
None
None
None
None