News-Details

News >Details

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA MKUNDI, MOROGORO

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA MKUNDI, MOROGORO

Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Mazingira kutoka Taasisi ya Taaluma za Maendeleo, Chuo Kikuu Mzumbe, kwa kushirikiana na wanataaluma wao, wametembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Mission to the Homeless Children , kilichopo eneo la Mkundi, Manispaa ya Morogoro tarehe 1 Juni 2025, kwa lengo la kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho. Akizungumza wakati wa kupokea ugeni huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Mission to the Homeless Children, Bw. Robert Simba, aliwapongeza wanafunzi kwa moyo wa kujitoa na kuonesha mfano wa vijana wenye maono ya kujenga jamii. “Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1996 kwa lengo la kuwapatia watoto hawa makazi salama, elimu na malezi bora. Mnaokuja na kuwakumbuka ni faraja kubwa kwao na kwetu,” alisema Bw. Simba. Katika ziara hiyo, wanafunzi hao walitoa msaada uliojumuisha vyakula, vifaa vya shule, vifaa vya usafi na taulo za kike, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kujenga jamii yenye mshikamano na huruma. Aidha, walishiriki michezo mbalimbali na watoto, kufanya usafi katika maeneo ya kituo na kushiriki furaha ya kula keki pamoja na watoto hao. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa kituo hicho, Bi. Faith Simba, aliwashukuru wanafunzi na uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa msaada walioutoa, akisisitiza kuwa msaada huo umeleta tabasamu kwa watoto na kutoa matumaini kwa maisha yao ya baadaye. “Tunaushukuru sana uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe na wanafunzi hawa kwa moyo wa upendo. Mmeonesha kuwa elimu sio tu darasani bali pia ni huduma kwa jamii,” alisema Bi. Faith Simba. Kwa upande wao, wanafunzi walieleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuiishi kaulimbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe isemayo: “Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu,”

None
None
None
None
None
None
None
None
None