News-Details

News >Details

KAMBI MAALUMU ZA UDAHILI CHUO KIKUU MZUMBE ZAVUTIA MAELFU NCHI NZIMA

KAMBI MAALUMU ZA UDAHILI CHUO KIKUU MZUMBE ZAVUTIA MAELFU NCHI NZIMA

Chuo Kikuu Mzumbe kimezindua rasmi huduma za udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kupitia kambi maalumu zilizowekwa katika mikoa mitano nchini Tanzania: Dodoma, Arusha, Mwanza, Dar es salaam na Mbeya. Hii ni sehemu ya juhudi za kukisogeza Chuo karibu na wananchi ikiwa ni sehemu ya kuiishi kaulimbiu yake isemayo: Chuo Kikuu Mzumbe, Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu. Huduma zinazotolewa katika kambi hizo ni pamoja na maelezo kuhusu sifa za kujiunga na programu mbalimbali, ushauri wa kitaaluma, pamoja na huduma ya udahili wa papo kwa hapo kwa ngazi zote za elimu: Astashahada, Stashahada, Shahada za Awali, Shahada za Umahiri, na Shahada za Uzamivu. Kambi hizo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi mbalimbali, wakiwemo wahitimu wa shule za sekondari, wazazi, walezi na wadau wa elimu wanaotafuta taarifa sahihi za kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe. Akizungumza wakati wa ziara yake katika banda la Mzumbe lililopo Dodoma, Bw. Noel John alisema amefurahishwa kuona Chuo hicho kimeamua kusogea karibu na wananchi. “Nimefarijika sana niliposikia tangazo kwamba Mzumbe wapo Dodoma. Hakika nimejiridhisha. Hii ni habari njema sana kwa vijana wetu,” alisema kwa furaha. Naye Bi. Hosanna Senoline, mhitimu wa kidato cha sita aliyefika katika banda la Mlimani City jijini Dar es Salaam, alipongeza elimu ya mwelekeo inayotolewa kwa wahitimu. “Elimu hii ya mwelekeo inayotolewa na Mzumbe ni msaada mkubwa kwa wahitimu ili kujiamulia maisha ya kitaaluma kwa uelewa wa kina. Ninawashauri wenzangu wasikose fursa hii,” alisisitiza Hosanna. Katika mkoa wa Mwanza, huduma hizo zimepokelewa kwa hamasa kubwa, huku wanafunzi na wazazi wakijitokeza kwa wingi katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe lililopo Rock City Mall. Mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda hilo, Asajile Abas, alisema kuwa amefaidika mno na elimu ya kitaaluma aliyoipata. “Nilikuwa sina uhakika ni kozi gani inanifaa kulingana na ufaulu wangu, lakini baada ya kupewa maelekezo na Maafisa wa Mzumbe, sasa nina mwelekeo mzuri wa kitaaluma. Nawashauri vijana wenzangu wa Mwanza wasikose hii nafasi,” alisema Asajile kwa matumaini. Tunawakaribisha wakazi katika mikoa yote ambayo Chuo Kikuu Mzumbe nimeweka kambi, kufika kupata huduma hizi muhimu. Maafisa mahiri kutoka Mzumbe wapo kuwahudumia kila siku kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni. Huduma zote hutolewa bila malipo na hakuna kiingilio. “Chuo Kikuu Mzumbe – Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu”

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None