News-Details

News >Details

MZUMBE YATOA SALAMU ZA POLE KWA WAKILI EVELYN KWEKA NA FAMILIA

MZUMBE YATOA SALAMU ZA POLE KWA WAKILI EVELYN KWEKA NA FAMILIA

Baadhi ya watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe hivi karibuni wameshiriki mazishi ya Baba mzazi wa Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo, Wakili Evelyn Kweka yaliyofanyika katika Kijiji cha Masama, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Miongoni mwa wawakilishi hao ni kutoka Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Idara ya Mipango, Ofisi ya Katibu wa Baraza la Chuo na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi. Kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha pamoja na jumuiya nzima ya Mzumbe, Dkt. Aloyce Gervas alitoa salamu za pole akisisitiza kuwa Chuo kipo pamoja na Wakili Kweka na familia yake katika kipindi cha majonzi. Katika salamu hizo, Dkt. Gervas alieleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinatambua na kuthamini mchango wa kila mtumishi na kwamba kushiriki katika nyakati kama hizo ni sehemu ya utamaduni wa taasisi katika kujenga mazingira ya kazi yenye utu, heshima na mshikamano wa kweli. Chuo Kikuu Mzumbe kinamuombea marehemu apumzike kwa amani na kuwaombea wafiwa wawe na moyo wa subira na faraja katika kipindi hiki.

None
None
None