News-Details

News >Details

CHUO KIKUU MZUMBE CHASHINDA TUZO KATIKA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI 2025

CHUO KIKUU MZUMBE CHASHINDA TUZO KATIKA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI 2025

Chuo Kikuu Mzumbe kimeibuka mshindi wa tatu katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki mwaka 2025, katika kundi la taasisi za mafunzo na utafiti. Tuzo hiyo inaashiria mafanikio ya Chuo katika kutoa elimu bora na mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya elimu na utafiti nchini. Tuzo hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda Burian, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Maonesho ya 32 ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Mjini Morogoro. “Utafiti na ubunifu wa kitaalamu ni nguzo muhimu katika kukuza sekta ya kilimo na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa letu,” alisema Balozi Dkt. Batilda Burian. Maonesho haya yamekuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau wa elimu, kilimo, mifugo uvuvi na maendeleo ya teknolojia. Maonesho haya yanafikia tamati leo tarehe 9 Agosti 2025 kwa ukanda wa mashariki iliyoshirikisha mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga.

None
None