News-Details

News >Details

MZUMBE WAENDELEZA UMAHIRI KATIKA KONGAMANO LA NNE LA MEL 2025

MZUMBE WAENDELEZA UMAHIRI KATIKA KONGAMANO LA  NNE LA MEL 2025

Chuo Kikuu Mzumbe kimeshiriki kikamilifu katika Kongamano la 4 la Kimataifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (Monitoring, Evaluation and Learning – MEL) linalofanyika tarehe 10–13 Septemba 2025 katika Hoteli ya Malaika Beach, Mwanza, likiwakutanisha wadau wa ndani na nje ya Tanzania. Mzumbe inashiriki kama taasisi kinara katika taaluma ya Ufuatiliaji na Tathmini inayotolewa chuoni kwa ngazi ya Shahada ya Awali na Shahada ya Umahiri. Washiriki wa chuo hicho, wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, wamehusika kikamilifu katika mijadala ya kitaaluma kuanzia siku ya kwanza ya kongamano hilo, lililofunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Dkt. Godfrey Kacholi ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi katika Shule ya Utawala wa Umma na Menejimenti na Mhariri Mkuu wa Jarida la Ufuatiliaji na Tathmini Katika Masuala ya Afya linalosimamiwa na Chuo Kikuu Mzumbe, ameongoza mjadala wa kwanza uliokuwa na mada kuhusu Agenda ya Ufuatiliaji Kutoka Afrika: Kuwezesha Watathimini Vijana na Wanaoiubukia Kuwa Mabingwa kwa ajili ya hali halisi ya Kiafrika yaani ‘The Made in Africa Evaluation Agenda: Empowering Young and Emerging Evaluators as Champions for a Context-driven Future’. Aidha Prof. Mackfallen Anasel ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Umahiri katika Ufuatiliaji na Tathimini kutoka Chuo Kikuu Mzumbe alikuwa ni sehemu ya wanajopo waliojadili mada kuhusu Tathimini Asilia kwa njia ya kukabiliana changamoto kutokan na Maarifa ya Jamii za Asili/Kienyeji katika Afrika, Amerika ya Kusini, Asia na Pasifiki yaani ‘Indigenous evaluation as approach to address complexity: Case study of Evallndigenous Experience in Africa, Latin America, Asia and Pacific’. Katika hatua nyingine mnamo tarehe 12 Septemba ,2025, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha anatarajiwa kutoa mada elekezi kuhusu DIRA 2050 na Mustakabali wa Uwezo wa Tathmini: Taasis za Elimu ya Juu Kama Kiini cha Mabadiliko yaani ‘DIRA 2050 and Future of Evaluation Capacity Higher Learning at the Core’. Kadhalika Wafanyakazi waendeshaji, Wanataaluma na Wanafunzi wa Skuli na Vitivo mbalimbali kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wameshiriki katika kongamano hilo.Chuo Kikuu Mzumbe kimeshiriki kikamilifu katika Kongamano la 4 la Kimataifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (Monitoring, Evaluation and Learning – MEL) linalofanyika tarehe 10–13 Septemba 2025 katika Hoteli ya Malaika Beach, Mwanza, likiwakutanisha wadau wa ndani na nje ya Tanzania. Mzumbe inashiriki kama taasisi kinara katika taaluma ya Ufuatiliaji na Tathmini inayotolewa chuoni kwa ngazi ya Shahada ya Awali na Shahada ya Umahiri. Washiriki wa chuo hicho, wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, wamehusika kikamilifu katika mijadala ya kitaaluma kuanzia siku ya kwanza ya kongamano hilo, lililofunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Dkt. Godfrey Kacholi ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi katika Shule ya Utawala wa Umma na Menejimenti na Mhariri Mkuu wa Jarida la Ufuatiliaji na Tathmini Katika Masuala ya Afya linalosimamiwa na Chuo Kikuu Mzumbe, ameongoza mjadala wa kwanza uliokuwa na mada kuhusu Agenda ya Ufuatiliaji Kutoka Afrika: Kuwezesha Watathimini Vijana na Wanaoiubukia Kuwa Mabingwa kwa ajili ya hali halisi ya Kiafrika yaani ‘The Made in Africa Evaluation Agenda: Empowering Young and Emerging Evaluators as Champions for a Context-driven Future’. Aidha Prof. Mackfallen Anasel ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Umahiri katika Ufuatiliaji na Tathimini kutoka Chuo Kikuu Mzumbe alikuwa ni sehemu ya wanajopo waliojadili mada kuhusu Tathimini Asilia kwa njia ya kukabiliana changamoto kutokan na Maarifa ya Jamii za Asili/Kienyeji katika Afrika, Amerika ya Kusini, Asia na Pasifiki yaani ‘Indigenous evaluation as approach to address complexity: Case study of Evallndigenous Experience in Africa, Latin America, Asia and Pacific’. Katika hatua nyingine mnamo tarehe 12 Septemba ,2025, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha anatarajiwa kutoa mada elekezi kuhusu DIRA 2050 na Mustakabali wa Uwezo wa Tathmini: Taasis za Elimu ya Juu Kama Kiini cha Mabadiliko yaani ‘DIRA 2050 and Future of Evaluation Capacity Higher Learning at the Core’. Kadhalika Wafanyakazi waendeshaji, Wanataaluma na Wanafunzi wa Skuli na Vitivo mbalimbali kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wameshiriki katika kongamano hilo.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None