News-Details

News >Details

MZUMBE MBIONI KUANZISHA KAMPASI MWANZA

MZUMBE MBIONI KUANZISHA KAMPASI MWANZA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema Mzumbe iko mbioni kuanzisha Kampasi mpya Mkoani Mwanza. Prof. Mwegoha ameyasema hayo tarehe 13 Januari 2025 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda. Amesema Chuo kimepata ekari 221 katika Wilaya ya Ilemela na kwa sasa mpango wa matumizi bora ya ardhi unaandaliwa. Akizungumza na sehemu ya Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza ni mkoa wa kimkakati na wapili kwa idadi kubwa na ongezeko la watu takribani milioni 3.6 na kutoa rai kwa Menejimenti kuanzisha kampasi mapema ili kuendana na mahitaji halisi ya mkoa kwa sasa. "Mwanza ni kitovu cha pili cha pato la taifa, tunakua kwa kasi sana. Mzumbe ni chuo chenye 'brand' kubwa oneni uwezekano wa kuanzisha kozi za kimkatati kwa kuzingatia mpango wa muda mfupi na muda mrefu" Katika ziara hiyo ya siku moja Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha pamoja na ujumbe wake pia amepata fursa ya kukutana na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Nyamiswi iliyopo Wilaya ya Ilemela Bw. Shija S. Mkangwa (Mwenyekiti wa Mtaa) na kuwahikishia mipango ya Serikali katika uanzishwaji wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mwanza

None
None
None
None
None
None