News-Details

News >Details

MZUMBE YAJIPAMBANUA KATIKA MAPINDUZI YA UJIFUNZAJI MSETO KUPITIA MRADI WA HEET

MZUMBE YAJIPAMBANUA KATIKA MAPINDUZI YA UJIFUNZAJI MSETO KUPITIA MRADI WA HEET

Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kuonesha dira ya ubunifu katika elimu ya juu nchini kupitia utekelezaji wa programu za ujifunzaji mseto (blended learning), ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET). Hayo yamebainishwa katika Warsha ya Tathmini ya Ujifunzaji Mtandaoni iliyofanyika leo tarehe 10 Oktoba 2025 katika Hoteli ya Morena, Morogoro. Akifungua warsha hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha, aliwataka wakuu wa idara kuwa chachu ya mageuzi ya kidijitali, akisisitiza kuwa wao ndio “farasi wa mbio katika safari ya mabadiliko ya elimu ya juu kwenye Vyuo Vikuu.” Alibainisha kuwa utekelezaji wa mageuzi hayo unatakiwa kuonekana katika ngazi za idara, ambako kazi ya kila siku ya kufundisha na kujifunza inafanyika. Pia, alihimiza kuwa Mradi wa HEET umeleta mageuzi makubwa katika miundombinu na teknolojia ya kujifunzia, sambamba na kujenga uwezo wa watumishi kitaaluma. “HEET haijengi tu miundombinu, bali inatengeneza misingi imara ya mabadiliko endelevu katika elimu ya juu,” alisisitiza. Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Hawa Tundui ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET alisisitiza umuhimu wa uratibu, ubunifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa programu hizo, akihimiza wakuu wa idara “kuonesha uongozi wa mfano na dhamira ya kweli katika mageuzi haya ya kidijitali.” Aliongeza kuwa mafanikio hayo yanachochewa na juhudi za Kituo cha Umahiri katika Ubunifu wa Ufundishaji na Ujifunzaji (Centre of Excellence in Innovative Teaching and Learning) ambacho kimekuwa kitovu cha ubunifu wa maudhui ya e-learning chuoni. Warsha hiyo imelenga kutathmini utekelezaji wa programu za ujifunzaji mseto, pamoja na kubaini mikakati endelevu ya kuboresha utoaji wa masomo kwa njia shirikishi na jumuishi, ili kuongeza ubora wa elimu na ushiriki wa wanafunzi katika zama hizi za kidijitali.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None