News-Details

News >Details

MZUMBE YAPIGA HATUA KATIKA MAANDALIZI YA MAUDHUI YA UJIFUNZAJI MSETO

MZUMBE YAPIGA HATUA KATIKA MAANDALIZI YA MAUDHUI YA UJIFUNZAJI MSETO

Chuo Kikuu Mzumbe kimeendesha mafunzo maalumu kwa kuhusu ujifunzaji mseto na uandaaji wa maudhui ya kidijitali kwa wanataaluma wa Chuo hichoo. Mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Magadu, Morogoro, kuanzia tarehe 20 Oktoba 2025 hadi 24 Oktoba 2025, yanalenga kuimarisha mbinu bora za ufundshaji mseto. Mafunzo hayo yanahusisha zaidi ya wanataaluma 125 kutoka kampasi zote za Chuo Kikuu Mzumbe. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Allen Mushi, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dira ya Chuo katika kuboresha ubora wa utoaji wa elimu kupitia matumizi ya teknolojia. “Hii ni wiki ya kazi. Ni wakati wa kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya kujifunzia vinapakiwa mtandaoni na viko katika mpangilio unaotakiwa. Tunapaswa kuanza kwa uthabiti kwa sababu namna tunavyoanza ndiyo itakayounda taswira ya kwanza ya ubora wetu,” amesisitiza Prof. Mushi. Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Umahiri katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kibunifu, Dkt. Perpetua Kalimasi ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwapa wahadhiri uelewa wa kina kuhusu mbinu za ujifunzaji mseto, pamoja na namna ya kuandaa na kupanga kozi mtandaoni kwa kutumia mfumo wa kujifunzia wa chuo. “Tunatarajia kila mshiriki atatoka hapa akiwa na uwezo wa kuandaa na kusimamia kozi zake mtandaoni kwa kutumia mfumo wa kujifunzia wa Mzumbe, ili wanafunzi waweze kujifunza kwa urahisi popote walipo,” Dkt. Kalimasi. Naye Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lihoya Chamwali amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya mwisho ya mradi huo unaotekelezwa katika Chuo Kikuu Mzumbe. “Kupitia mradi wa HEET, chuo kimefanikiwa kupitia upya jumla ya mitaala 53 na kuanzisha programu mpya 11 za uzamili zinazotolewa kwa mfumo wa ujifunzaji mseto. Hadi sasa, programu hizo zimeidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na wanafunzi wanatarajiwa kuanza masomo yao hivi karibuni,” Dkt. Chamwali. Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dkt. Mustapha Almasi, ameongoza mafunzo kwa washiriki kuhusu mapitio ya miundo ya kozi na upangaji sahihi wa maudhui kulingana na mahitaji ya wanafunzi wa kidijitali. Kupitia mafunzo haya, Chuo Kikuu Mzumbe kinaendelea kuweka msingi thabiti wa mabadiliko kuelekea elimu ya kisasa inayozingatia ubunifu, ushirikishwaji na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None