News-Details

News >Details

BW. GODLOVE BARIKIEL AFANIKIWA KUTETEA TASNIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

BW. GODLOVE BARIKIEL AFANIKIWA KUTETEA TASNIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kudhihirisha ubora katika kukuza tafiti zenye mchango kwa maendeleo ya Taifa na jamii baada ya Bw. Godlove Barikiel, mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Taasisi ya Taaluma za Maendeleo (IDS), kufanikiwa kutetea tasnifu yake tarehe 6 Novemba 2025, katika Kampasi Kuu ya Morogoro. Utetezi huo umefanyika mbele ya jopo la watahini lililoongozwa na Mwenyekiti Profesa Frank Theobald Theodory, huku Profesa Elizabeth Lulu Genda akiwa Msimamizi Mkuu wa utafiti na Dkt. Moses Ndunguru Msimamizi Msaidizi. Tasnifu ya Bw. Barikiel imechunguza kwa kina namna vitendo vya ukatili wa wapenzi vinavyoathiri uwezo wa waathirika kupanga, kutumia, na kuhifadhi rasilimali za familia kwa ufanisi. Kupitia matokeo ya utafiti wake, Bw. Barikiel alisisitiza umuhimu wa kuimarisha msaada kwa waathirika wa ukatili wa nyumbani, kukuza elimu ya usimamizi wa rasilimali, na kuboresha sera zinazolenga ustawi wa familia na jamii. Baada ya majadiliano ya kina, Prof. Theodory alimtangaza rasmi Bw. Barikiel kuwa amefaulu kutetea tasnifu yake ya Uzamivu, akibainisha kuwa utafiti huo una mchango mkubwa katika kuboresha ustawi wa familia na kuimarisha maisha ya waathirika wa ukatili wa nyumbani nchini. Kupitia mafanikio haya, Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kuthibitisha nafasi yake kama kitovu cha tafiti bunifu na zenye mchango chanya kwa maendeleo endelevu ya jamii na taifa kwa ujumla.

None
None
None
None
None
None
None
None