News-Details

News >Details

MZUMBE YADHIHIRISHA UBORA WA HALI YA JUU KATIKA MAHAFALI YA 24 ya CHUO HICHO

MZUMBE YADHIHIRISHA UBORA WA HALI YA JUU KATIKA MAHAFALI YA 24 ya CHUO HICHO

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewatunuku jumla ya wanachuo 5,091 kutoka Astashahada hadi Shahada za Uzamivu, ongezeko la asilimia 6.7 ukilinganisha na mwaka jana hatua inayothibitisha hadhi yake kama moja ya taasisi bora za elimu ya juu nchini baada ya kutangaza ongezeko kubwa la ubora wa elimu, utafiti na miundombinu. Akizungumza katika mahafali ya 24 ya Chuo hiyo yaliyofanyika tarehe 20 Novemba 2025 katika eneo la Maekani Kampasi Kuu Morogoro, Mhe. Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususani katika kuimarisha elimu ya juu na utafiti na kuwawataka wahitimu kuwa wawakilishi wazuri wa Chuo Kikuu Mzumbe na kuitumikia jamii kwa weledi na maadili Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Saida Yahya Othman, amesisitiza ujumbe huo na kuwataka wahitimu kuzingatia maadili, ubunifu na nidhamu katika maisha yao ya kitaaluma na kijamii. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, amesema katika kundi maalumu la wahitimu wa Shahada ya Uzamivu (PhD), mwaka huu wamehitimu wanachuo 15, ikilinganishwa na 12 wa mwaka jana miongoni mwao yumo Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, hatua inayoifanya Mzumbe kujivunia mchango wake katika kuwaandaa wataalamu na viongozi wa juu wa nchi. Prof, Mwegoha amefafanua kuwa maendeleo yaliyofikiwa na chuo katika nyanja za elimu, utafiti, ushirikiano na miundombinu kupitia mradi wa HEET na miradi ya ndani. Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendeleza uwekezaji katika elimu ya juu na kuwashukuru wazazi, wadau na viongozi waliolishiriki tukio hilo. Katika kutambua ubora wa wanafunzi, Mzumbe imemtangaza Bi. Melina Baradyana, mwanafunzi wa Shahada ya Usimamizi wa Mazingira, kuwa Mwanafunzi Bora wa Kampasi Kuu, kutokana na umahiri wa kitaaluma na nidhamu ya mfano. Bi. Melina amepata WAKIA (GPA) wa 4.8, ukiwa ni ufaulu wa juu zaidi kuliko wanafunzi wengine. Awali, Mlau wa Mahafali hayo, Prof. Lulu Genda, amewataka wahitimu kuwa mfano mwema katika jamii wanazokwenda kuzitumikia, huku akisisitiza: “Elimu ni bahari isiyotulia; msikubali kubebwa na mawimbi. Fikirini kwa kina, tafuteni maarifa mapya kila siku, na tumieni hekima yenu kwa manufaa ya jamii. Kila hatua ya elimu ni nafasi ya kuendeleza ujuzi na kuchangia maendeleo ya nchi.” Chuo Kikuu Mzumbe kinawakaribisha wananchi na wadau kuungana katika sherehe mbili zilizobaki, tarehe 27 Novemba 2025 katika Ndaki ya Mbeya na tarehe 4 Disemba 2025 katika Ndaki ya Dar es Salaam, kikisisitiza falsafa yake: “Mzumbe – Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu.”

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None