News-Details

News >Details

WANATAALUMA WA NDAKI YA MBEYA WANOLEWA KWENYE MAFUNZO YA STADI ZA MSINGI

WANATAALUMA WA NDAKI YA MBEYA WANOLEWA KWENYE MAFUNZO YA STADI ZA MSINGI

Chuo Kikuu cha Mzumbe, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kimeendesha mafunzo ya stadi za msingi kwa wanataaluma wa Ndaki ya Mbeya tarehe 9 Januari 2025, Jijini Mbeya. Mafunzo hayo ya siku mbili yalilenga kuwaimarisha wanataaluma katika nyanja za ufundishaji, utafiti na utoaji wa huduma kwa jamii. Akifungua mafunzo hayo, Naibu Rasi wa Ndaki ya Mbeya, Prof. Charles Tundui, aliwashukuru waratibu wa HEET kwa kuandaa mafunzo hayo na kusisitiza kuwa Ndaki ya Mbeya inathamini jitihada za kuimarisha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji. Mada zilizowasilishwa zilihusisha mbinu bora za ufundishaji vyuo vikuu, stadi za mawasiliano, tathmini na usimamizi wa tafiti za wanafunzi, matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji, pamoja na uadilifu wa kitaaluma. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha TEHAMA na Mratibu wa Mradi wa HEET upande wa mifumo ya kidigitali, Dkt. Mohamed Ghasia, alieleza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ubora wa elimu ya juu kwa kujenga uwezo wa wanataaluma ili kukidhi mahitaji ya mazingira ya sasa ya elimu. Aidha, Mhadhiri Mwandamizi na Mratibu wa HEET upande wa Kituo cha Ubora katika Ufundishaji na Ujifunzaji, Dkt. Perpetua Kalimasi, alisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo katika kuhakikisha Chuo Kikuu Mzumbe kinazalisha wahitimu wenye uwezo wa kutatua changamoto za jamii. Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba, Dkt. Kardo Mwilongo, aliwasilisha mada ya Elimu Mtandao na kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo ya kujifunzia. Naye Dkt. Mustapha Almasi alisisitiza matumizi ya mbinu bunifu za ufundishaji katika ulimwengu wa kidigitali unaojumuisha matumizi ya akili unde. Washiriki walieleza kuridhishwa na mafunzo hayo na kuomba yaendelezwe mara kwa mara ili kuendelea kuimarisha ubora wa elimu Chuoni.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None