News-Details

News >Details

MZUMBE YATHAMINI MCHANGO WA BARAZA LA 9 KATIKA MAENDELEO YA CHUO

MZUMBE YATHAMINI MCHANGO WA BARAZA LA 9 KATIKA MAENDELEO YA CHUO

Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia Menejimenti yake leo tarehe 31 Januari 2026, imewaaga rasmi Wajumbe wa Baraza la 9 la Chuo, linalohitimisha rasmi kipindi chake cha kusimamia utekelezaji wa shughuli za chuo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kutambua na kuthamini mchango wa Baraza hilo katika maendeleo ya Chuo. Baraza la 9 la Chuo liliongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Saida Yahya-Othman, ambaye katika uongozi wake ameendelea kusisitiza misingi ya utawala bora, maamuzi ya kimkakati na usimamizi madhubuti wa ubora wa taaluma, utafiti na huduma kwa jamii katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu ya Baraza. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na sehemu ya Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, ambaye alitoa pongezi na kulishukuru Baraza kwa mchango wake mkubwa katika kuisimamia dira ya Chuo na kushauri Menejimenti katika masuala muhimu ya maendeleo ya taasisi. Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mwegoha alisema Baraza la 9 limeacha alama chanya katika historia ya Chuo Kikuu Mzumbe, hususan katika kuimarisha mifumo ya uongozi, kusimamia mageuzi ya kitaasisi na kulinda hadhi ya Chuo kama taasisi ya elimu ya juu yenye mchango mkubwa kwa Taifa. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la 9, Prof. Saida Yahya-Othman, aliishukuru Menejimenti ya Chuo kwa ushirikiano na mshikamano uliokuwepo katika kipindi chote cha uongozi wa Baraza, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza maadili, uwajibikaji na ubora kama misingi ya maendeleo endelevu ya Chuo Kikuu Mzumbe. Hafla hiyo fupi ilihitimishwa kwa kutolewa kwa shukrani na salamu za heri kwa wajumbe wa Baraza linalomaliza muda wake, ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango katika kukitumikia Chuo.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None