News-Details

News >Details

BARAZA LA WAFANYAKAZI MZUMBE LATATHMINI MAENDELEO YA CHUO NA USTAWI WA WATUMISHI

BARAZA LA WAFANYAKAZI MZUMBE LATATHMINI MAENDELEO YA CHUO NA USTAWI WA WATUMISHI

Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora na ushirikishwaji wa watumishi kupitia mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo, tarehe 11 Februari 2026, jijini Tanga mkutano ambao uliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo. Mkutano huo muhimu umelenga kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu maendeleo ya chuo na wafanyakazi wake, ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za uongozi wa chuo kuhakikisha Mzumbe inaendelea kuwa taasisi bora ya elimu ya juu inayokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa. Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa ni Taarifa ya Miradi ya Maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe, ambapo wajumbe walipata fursa ya kufahamu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayolenga kuboresha miundombinu, mazingira ya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii. Aidha, Mkutano huo ulipokea na kujadili kwa kina Taarifa ya Maendeleo ya Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwezi Mei, 2025 hadi Januari, 2026, taarifa iliyobainisha mafanikio yaliyopatikana katika masuala ya ajira, mafunzo na maendeleo ya watumishi, upandishwaji vyeo, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wake. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Prof. Mwegoha alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa pamoja wa wafanyakazi wote katika kujenga chuo chenye mwelekeo wa maendeleo endelevu, akibainisha kuwa mafanikio ya Mzumbe yanategemea kwa kiasi kikubwa mshikamano, uwajibikaji na ubunifu wa kila mmoja. Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Idara, Kurugenzi, Skuli, Vitivo na Ndaki zote za Chuo Kikuu Mzumbe, hali iliyoonesha uwakilishi mpana na mshikamano wa pamoja katika kujadili masuala yanayogusa mustakabali wa chuo na wafanyakazi wake. Kwa ujumla, maazimio na mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano huo yanatarajiwa kutafsiriwa katika hatua za utekelezaji zitakazochochea maendeleo ya chuo, kuboresha maslahi ya wafanyakazi, na kuimarisha nafasi ya Chuo Kikuu Mzumbe kama taasisi kinara wa elimu ya juu nchini.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None