News-Details

News >Details

MZUMBE WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KIKAO KAZI CHA SITA CHA SERIKALI MTANDAO

MZUMBE WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KIKAO KAZI CHA SITA CHA SERIKALI MTANDAO

huo Kikuu Mzumbe kimeungana na taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi kushiriki katika Kikao kazi cha 6 cha Serikali Mtandao, kinachofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Februari 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC). Kikao hicho kinaongozwa na kaulimbiu, “Kuboresha Utendaji wa Serikali kwa Kuimarisha Utoaji wa Huduma za Umma kupitia Mifumo Salama na Jumuishi ya Serikali Mtandao,” kikilenga kujadili ufanisi, maendeleo, mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini. Akifungua kikao hicho, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amepongeza taasisi za umma kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika matumizi ya teknolojia za kidijitali katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Amesema mifumo ya Serikali Mtandao imeongeza uwazi, ufanisi, uwajibikaji na kasi ya utoaji huduma, huku ikiimarisha ushirikiano wa taasisi kupitia mifumo iliyounganishwa. Aidha, amesisitiza kuimarishwa kwa usalama wa mifumo ya TEHAMA, ubunifu katika huduma za kidijitali, ujenzi wa uwezo wa rasilimali watu, na kuendeleza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, hususan watoa huduma za kidijitali, ili kuhakikisha huduma zinakuwa jumuishi na endelevu. Chuo Kikuu Mzumbe kinashiriki kikamilifu kama miongoni mwa taasisi vinara katika matumizi ya mifumo tumizi ya serikali. Kimechangia wataalamu katika timu za usanifu na uendelezaji wa mifumo ya kidijitali ya serikali, hatua inayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma za umma. Katika hatua nyingine, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Irene Isibika, ameongoza mjadala kuhusu Serikali ya Kidijitali katika Viwango vya Juu: Michakato Muhimu ya Kibiashara ya Serikali Kuu katika Mfumo wa Kidijitali. Ushiriki wa Chuo unaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kuendeleza matumizi ya TEHAMA na kuchangia juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kidijitali na utawala bora.

None
None
None
None
None
None
None
None
None