News-Details

News >Details

CHUO KIKUU MZUMBE CHAKABIDHI VIFAA VYA KUTENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI KWA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI (LEVO NA MOROGORO PARALEGAL CENTRE)

CHUO KIKUU MZUMBE CHAKABIDHI VIFAA VYA KUTENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI KWA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI (LEVO NA MOROGORO PARALEGAL CENTRE)

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Maudhui mafupi ya KITEHAMA hii leo umekabidhi vifaa vyenye thamani ya takriban Milioni Thelathini kwa taasisi ya Legal Vision Organisation (LEVO) ya Lushoto - Tanga) na Morogoro Paralegal Centre (MPLC -Morogoro) katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Lushoto, Mkoani Tanga. Akikabidhi vifaa hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo Kikuu Mzumbe kama yalivyoainishwa kwenye Mpango mkakati wa Chuo, yaani Kufundisha, kufanya tafiti zenye tije, na kutoa ushauri wa kitaalamu. “Mradi huu unajumuisha dhamira ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa maono na dhamira yake ya kushughulikia mahitaji muhimu ya jamii, hususani suala la elimu ya kisheria kwa umma na upatikanaji wa haki hasa kwa makundi yenye uhitaji zaidi, wakiwemo watu wenye hali ngumu ya kiuchumi, wanawake, watoto na walemavu, ambao hawawezi kumudu gharama za uwakilishi wa mawakili binafsi” Amesitiza Prof. Mwegoha. Awali Mratibu wa Mradi Bw. Edger Rutatola amesema wasaidizi wa kisheria wana jukumu muhimu katika kutoa suluhisho la kivitendo la kuimarisha upatikanaji wa haki, kutoa ushauri wa kimsingi wa kisheria, elimu ya kisheria, kuwezesha upatanishi na utatuzi mbadala wa migogoro, kutetea haki za binadamu, na kutoa uhamasishaji wa jamii kuhusu sheria, hasa haki na wajibu wa raia kikatiba na sheria za nchi. “Kwa kuwapatia wasaidizi wa kisheria uwezo wa kutengeneza maudhui ya kitehama, tunawawezesha kuwafikia watu wengi zaidi na ufanisi mkubwa zaidi. Chuo Kikuu Mzumbe kinatambua umuhimu wa ushirikiano katika kufikia malengo yake. Hivyo, mradi huu unafanya kazi kwa karibu na wasaidizi wa kisheria katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.” Amesisitiza Bw. Rutatora Hakimu Mkazi wa wilaya ya Lushoto Mhe. Rose Ngoka amesema taasisi ya LEVO wilayani Lushoto imekuwa na msaada mkubwa katika kutatua migogoro kwa njia ya amani. Katika Wilaya ya Lushoto maudhui ya mtandaoni yamesambazwa katika Mabasi, Shule za Sekondari, Hospitali na Vituo vya Afya, Kumbi za starehe na kambi za elimu.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None