News-Details

News >Details

MWANAFUNZI WA MZUMBE BI. PRISILA KESSY AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA TEHAMA 2025

MWANAFUNZI WA MZUMBE BI. PRISILA KESSY AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA TEHAMA 2025

Mwanafunzi wa masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Prisila Emmanuel Kessy ameibuka mshindi na kutwaa tuzo mbili za ubunifu kwenye masuala ya TEHAMA zilizoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA. Katika hafla ya ugawaji wa tuzo hizo iliyofanyika Februari 21, 2025 katika Hotel ya Gran Meliá jijini Arusha, Bi. Kessy ametajwa kuwa mshindi wa nafasi ya kwanza katika kipengele cha "Young ICT Achiever - Student Entrepreneur" na Mshindi wa Tatu (Third Runner-Up) katika Tuzo ya "Women in ICT - Female Innovator" ikiwa ni ushuhuda wa kipaji chake, juhudi zake, na mchango wake katika sekta ya TEHAMA. Chuo Kikuu Mzumbe kimempongeza Bi Kessy kwa mafanikio hayo makubwa na kueleza kuwa kitaendelea kuinua vipaji vingi zaidi vya ubunifu kupitia kituo chake cha ulezi na uatamizi wa bunifu kinachoendeshwa chini ya Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Uhusiano ya Kitasnia. “Tunajivunia sana mafanikio ya Mwanafunzi wetu Bi. Kessy kwani hatua hii inaleta hamasa kwa wanafunzi na vijana wengine wenye ndoto za kuleta mabadiliko katika teknolojia na biashara. Chuo Kikuu Mzumbe tunalea mawazo ya kibunifu na biashara kupitia kituo maalumu ambacho ni huru kwa wanafunzi wote na Prisila amelelewa katika kituo hicho na leo tunashuhudia akipeperusha bendera ya chuo kwa mafanikio haya makubwa tunampongeza na kujivunia sana.” Alisema Bi.Lulu Mussa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa chuo kikuu Mzumbe. Ameongeza kuwa mafanikio ya Bi. Kessy ni ushuhuda kuwa kizazi kipya cha Tanzania hususani wasichana wanayo fursa kubwa katika kuendeleza sekta ya TEHAMA ikiwa watalelewa na kupatiwa miongozo vizuri na amewakaribisha Wanafunzi wanaopenda kusomea masomo ya TEHAMA kujiunga na chuo hicho kwani kimebobea pia kwenye upande wa Sayansi na kinazo kozi nyingi katika kitivo cha Sayansi na Teknolojia (FST)

None
None
None
None