News-Details

News >Details

CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI TANZANIA WAJIFUNZA KUHUSU MASWALA YA UTHIBI UBORA KWA CHU KIKUU MZUMBE

CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI TANZANIA WAJIFUNZA KUHUSU MASWALA YA  UTHIBI UBORA KWA CHU KIKUU MZUMBE

Chuo cha mafunzo ya kijeshi Tanzania (TMA) kimefanya ziara ya kujifunza kuhusu uthibiti ubora - Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Kitengo Cha Uthibiti Ubora kwa lengo la kujifunza mifumo ya ndani ya usimamizi wa ubora inayotekelezwa na chuo hicho. Ziara hiyo imefanyika Aprili 30, 2026 katika Kampasi Kuu, Morogoro. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lawrencia Mushi, aliwakaribisha wageni hao na kuwapatia maelezo kuhusu namna chuo kinavyosimamia na kuratibu masuala ya Uthibiti Ubora. Alieleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kina mifumo madhubuti ya kuhakikisha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, utafiti na utoaji wa huduma kwa Jamii unazingatia viwango vya kitaifa na kimataifa. Akizungumza pia katika kikao hicho, Mratibu wa Uthibiti Ubora wa maswala ya Taaluma, Utafiti na Ushauri Dkt. Bahati Ilembo, alifafanua muundo wa mfumo wa uthibiti ubora wa chuo, akibainisha kuwa Kitengo cha Uthibiti Ubora kina jukumu la kuratibu masuala yote ya ubora katika Kampasi, Shule, Vitivo na Taasisi zote za chuo, zikiwemo Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam, huku mipango ikiendelea ya kuanzisha Kampasi ya Tanga. Ameongeza kuwa katika kila kitengo kuna waratibu wa uthibiti ubora wanaosaidia kusimamia utekelezaji wa viwango vilivyowekwa. Aidha, Dkt. Ilembo alisisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo ya taasisi za udhibiti kama Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania pamoja na miongozo ya kikanda kutoka Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki, akieleza kuwa chuo kimekuwa kikihakikisha kinazingatia viwango hivyo katika utekelezaji wa shughuli zake, ikiwemo matumizi ya mifumo ya ufundishaji wa Mseto. Kwa ujumla, ziara hiyo ya kujifunza inatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya Chuo cha Mafunzo ya kijeshi Tanzania na Chuo Kikuu Mzumbe, katika kuimarisha mifumo ya ndani ya uthibiti ubora, hatua itakayochangia kuboresha utoaji wa elimu na huduma bora katika taasisi hizo.

None
None
None
None
None
None