News-Details

News >Details

MZUMBE YAJENGA UWEZO WA WATAALAMU WA MPANGO WA TAIFA WA CHANJO

MZUMBE YAJENGA UWEZO WA WATAALAMU WA MPANGO WA TAIFA WA CHANJO

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Idara ya Menejimenti ya Mifumo ya Afya, Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti kimeendesha Mafunzo ya Kujenga Uwezo katika Uongozi, Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini kwa wataalamu 55 wa Mpango wa Taifa wa Chanjo. Mafunzo hayo yanaendelea jijini Arusha kwa siku tano kuanzia Mei 18 hadi 22, 2026, yakihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Afya - Mpango wa Taifa wa Chanjo. Akifungua mafunzo hayo Mgeni Rasmi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Otilia Gowelle amesema serikali inaendelea kujenga uwezo wa wataalamu wake ili kuhakikisha huduma za chanjo zinawafikia wananchi kwa ubora na kwa wakati sambamba na kuimarisha mifumo ya afya inayoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali. Aliwahimiza washiriki kutumia mafunzo hayo kuboresha utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano katika kufanikisha malengo ya taifa ya kuongeza huduma za chanjo na kulinda afya ya jamii. Awali akitoa maelezo ya utangulizi, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dkt. Georgina Joachim, alisema programu ya chanjo inahitaji mifumo imara ya uratibu na ufuatiliaji ili kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uwajibikaji, kuboresha utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa programu hiyo. Kwa upande wake, Amidi wa Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Idda Lyatonga Swai amesema Chuo kina uzoefu mkubwa katika utoaji wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalamu waliopo kazini pamoja na kuandaa wataalamu wapya. Alibainisha kuwa ushirikiano kati ya Chuo na Wizara ya Afya umewezesha utekelezaji wa mafunzo, tafiti na uandaaji wa Sera mbalimbali yenye tija kwa sekta ya afya. Mafunzo haya yanaendeshwa na Wawezeshaji Chuo Kikuu Mzumbe akiwemo, Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mifumo ya Afya, Prof. Mackfallen Anasel, Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Godfrey Kacholi na Mkufunzi Msaidizi Bw. Mzakiru Twalibu, wakijikita katika mada kuhusu Uongozi wa Maadili na Usimamizi Bora kwa Utawala wa Uwajibikaji na Uwazi katika Programu za Afya, Usimamizi wa Migogoro na Utatuzi wa Migogoro, Ugawaji wa Majukumu, Makabidhiano ya Kazi, na Usimamizi wa Muda, pamoja na Muundo wa Mifumo ya Afya na Fikra za Kimfumo katika Afya wakati wa Mafunzo hayo Mafunzo haya ni matokeo ya mahusiano mazuri kati ya taasisi hizo mbili na yatasaidia kuboresha utendaji kazi, kuongeza uwajibikaji na kuimarisha ushirikiano katika ngazi mbalimbali za utekelezaji wa programu za chanjo nchini

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None