News-Details

News >Details

PROF. MWEGOHA ATOA WITO WA MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA NDAKI YA DAR ES SALAAM

PROF. MWEGOHA ATOA WITO WA MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA NDAKI YA DAR ES SALAAM

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amewataka watumishi wa Ndaki ya Dar es Salaam kuendelea kudumisha mshikamano, uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuimarisha zaidi hadhi, taswira na maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe. Hayo yamejiri wakati wa kikao maalumu kilichofanyika tarehe 25 Mei 2026 katika Ndaki ya Dar es Salaam kilichowakutanisha viongozi na watumishi wa ndaki hiyo kwa lengo la kujadili maendeleo ya Chuo, ustawi wa watumishi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi na utoaji huduma. Akizungumza katika kikao hicho, Prof. Mwegoha amesema kuwa kila mtumishi ana nafasi muhimu katika kuijenga taasisi kupitia utendaji kazi wenye ufanisi, nidhamu, kujituma na ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu ya kila siku. Ameeleza kuwa mafanikio ya Chuo Kikuu Mzumbe yanategemea jitihada za pamoja za watumishi wa kada zote, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa moyo wa kujitolea na kuwajibika kwa manufaa ya taasisi na jamii kwa ujumla. Aidha, Prof. Mwegoha amewahimiza watumishi kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zinazojitokeza mahali pa kazi na kutumia fursa mbalimbali zilizopo kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanafunzi, wadau na jamii. Amesema mazingira bora ya kazi na mahusiano mazuri baina ya watumishi ni msingi muhimu wa kuongeza tija na kuifanya Mzumbe kuendelea kuwa miongoni mwa vyuo vinavyoongoza nchini katika utoaji wa elimu ya juu. Katika hatua nyingine, Prof. William Mwegoha amepongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa Ndaki ya Dar es Salaam katika kuimarisha mazingira ya kufundishia, kujifunzia na kufanyia kazi, huku akibainisha kuwa juhudi hizo zinaendelea kuongeza ubora wa huduma na kuimarisha mazingira ya kitaaluma ndani ya Chuo. Kwa upande wao, viongozi mbalimbali wa Chuo waliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Chuo, maendeleo ya miundombinu pamoja na mipango ya kimkakati inayolenga kuendelea kukikuza Chuo Kikuu Mzumbe kitaaluma na kiutendaji. Viongozi hao pia waliwahamasisha watumishi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha malengo ya taasisi kwa kuzingatia uwajibikaji, ubunifu na ushirikiano katika maeneo yao ya kazi. Kikao hicho kilihitimishwa kwa wito wa pamoja wa kuendeleza nidhamu ya kazi, mshikamano na uwajibikaji miongoni mwa watumishi, hatua inayotarajiwa kuimarisha zaidi ufanisi wa utendaji na kuchochea maendeleo endelevu ya Chuo Kikuu Mzumbe katika nyanja za kitaaluma, kiutawala na utoaji huduma kwa wadau wake.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None