News-Details

News >Details

PROF. MWEGOHA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI KAMPASI MPYA - TANGA

PROF. MWEGOHA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI KAMPASI MPYA - TANGA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo hicho katika Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Prof. William Mwegoha ameyasema hayo leo Februari 26, 2025 mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo na hatua za mradi wa ujenzi katika eneo la Gombero, Wilayani Mkinga. “Nimeridhika na kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi mzawa wa Dimetoclasa Real Hope pamoja na mshauri elekezi ambao wanafanya kazi kwa kushirikiana na leo hii mradi umefikia asilimia 36 ikiwa uko mbele ya mpango kazi kwa siku kumi na moja” Amesisitiza Prof. Mwegoha Amemtaka Mkandarasi huyo kuzingatia viwango vya ubora kuanzia hatua za ujenzi mpaka ukamilishaji wake kwani ni mradi wa kimkakati. Pia amewataka kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na jamii inayozunguka mradi huo kwa kuwa wao ndio walinzi wakubwa wa miundombuni hiyo. “Endeeleeni kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Serikali kuanzia Mkoa, Wilaya hadi ngazi ya kijiji kwa kuwa tunapata uimarishaji wa miundombinu yote ikiwa ni pamoja na barabara na umeme, vimefikishwa mpaka eneo hili na Serikali” Aidha, amemtaka Mkandarasi kuendelea kuzingatia kikamilifu sheria, taratibu na kanuni za usalama mahala pa kazi na kutoa msukumo kwa juu ya masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira. Awali Kaimu Msimamizi wa Ujenzi Bw. Joseph Ng'wala amesema ujenzi wa Lot 1 unahusisha jengo la Taaluma, Kituo cha Afya na Mgahawa wakati Lot 2 inahusisha ujenzi wa mabweni ya wasichana na wavulana, nyumba za watumishi, miundombinu ya maji safi na maji taka. Kukamilika kwa mradi huu itakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo Kikuu Mzumbe kama yalivyoainishwa kwenye Mpango mkakati wa Chuo, yaani Kufundisha, kufanya tafiti zenye tija na kutoa ushauri wa kitaalamu.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None