News-Details

News >Details

MAAFISA KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO WANOLEWA KATIKA MAFUNZO YANAYOHUSU MAJUKUMU YAO

MAAFISA KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO WANOLEWA   KATIKA MAFUNZO YANAYOHUSU MAJUKUMU YAO

Watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wamepatiwa mafunzo maalumu yaliyolenga kuimarisha ufanisi wa shughuli za masoko na mawasiliano ya taasisi hiyo. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 1 Aprili 2026 katika ukumbi wa Morena, yakihusisha maafisa masoko, maafisa mawasilano na maafisa TEHAMA kutoka Kampasi Kuu, Kampasi ya Mbeya na Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bi. Lulu Mussa alieleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo na kukuza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Kitengo hicho jambo ambalo litachochea kujenga taswira chanya ya Chuo Kikuu Mzumbe kwenye jamii na kuhakikisha wadau wote wanapata taarifa sahihi zinazohusu Chuo kwa wakati. Aidha, Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Prof. Omary Swalehe aliwasilisha mada kuhusu Mikakati ya Masoko na Matangazo Kidigitali huku akisisitiza washiriki umuhimu wa utafiti wa masoko katika kubaini mahitaji ya wadau, pamoja na kubuni maudhui yenye mvuto na yanayolenga matokeo. Mafunzo hayo pia yaligusia dhana ya mawasiliano jumuishi inayohakikisha kuwa ujumbe wa taasisi unakuwa thabiti katika majukwaa yote ya mawasiliano na matumizi ya majukwaa ya kidigitali ikiwemo mitandao ya kijamii. Aidha, Afisa Ununuzi Mwandamizi kutoka Kitengo cha Ununuzi cha Chuo Kikuu Mzumbe, Bw. Salum Mpindamila, aliwasilisha mada kuhusu utendaji kazi na matumizi ya Mfumo wa NeST (National e-Procurement System) pamoja na usimamizi wa mikataba kwa washiriki wa mafunzo maalumu kutoka Kitengo cha Mawasiliano na Masoko cha Chuo Kikuu Mzumbe. Katika uwasilishaji wake, Bw. Mpindamila alieleza kwa kina namna ya kutumia mfumo wa NeST katika kurahisisha taratibu za ununuzi wa umma, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo ya mfumo huo ili kuongeza uwazi na uwajibikaji. Kwa upande wao, washiriki walieleza kuridhishwa na mafunzo hayo, wakibainisha kuwa yamewapa maarifa mapya yatakayowawezesha kuboresha utendaji wao wa kila siku. Walisisitiza umuhimu wa kuendeleza mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mienendo ya mawasiliano duniani. Mafunzo hayo ni kielelezo kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimejipanga na kinahakikisha kuwa wadau wote watapata huduma bora kutoka kwa watumishi waliojengewa uwezo na wenye ushindani kwa ajili ya maendeleo ya taasisi. https://www.instagram.com/p/DWnqVzjgkG9/?img_index=3&igsh=NWs3MTVjMXM1YjJr

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None