News-Details

News >Details

WAJUMBE WA MENEJIMENTI YA MZUMBE WANOLEWA KATIKA USIMAMIZI WA UNUNUZI WA UMMA KUPITIA MFUMO WA NeST

WAJUMBE WA MENEJIMENTI YA MZUMBE WANOLEWA KATIKA USIMAMIZI WA UNUNUZI WA UMMA KUPITIA MFUMO WA NeST

Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe wameanza rasmi mafunzo maalumu ya siku tatu yanayohusu Usimamizi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (PPA), Matumizi ya Mfumo wa NeST (National e-Procurement System) na Usimamizi wa Mikataba. Akifungua mafunzo hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Allen Mushi amewataka washiriki kuzingatia mafunzo haya kwa makini kwani yatakuwa na manufaa makubwa katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na usimamizi wa rasilimali ndani ya taasisi. Prof. Mushi amesisitiza kuwa mfumo wa NeST ni nyenzo muhimu katika kuboresha michakato ya ununuzi na kuongeza uwazi na usahihi katika utekelezaji wa miradi, hivyo kila mshiriki atapata faida kubwa katika kuelewa matumizi ya mfumo huu wa kisasa. Awali, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bw. Castor Komba, alieleza kuwa mafunzo haya yamelenga kuwajengea washiriki uwezo wa kutumia mfumo wa NeST huku wakipata uelewa wa kina kuhusu sheria na taratibu za ununuzi wa umma pamoja na usimamizi wa mikataba. Aidha, Mtoa mada Bw. Anthony Masau kutoka PPRA alieleza kwa kina kuhusu mfumo wa NeST akibainisha vipengele muhimu vinavyorahisisha mchakato wa ununuzi ndani ya taasisi za umma. Alifafanua jinsi mfumo huu unavyowezesha uratibu mzuri wa mahitaji ya idara, ikiwa ni pamoja na tathmini ya bajeti, kiasi kinachohitajika, na uteuzi wa huduma. Pia, aligusia namna mfumo huo unavyorahisisha ununuzi wa thamani ndogo, pamoja na ununuzi baina ya Taasisi za Kiserikali kwa kuhakikisha kuwa kila hatua inafuata taratibu rasmi na kuepusha kasoro zinazoweza kujitokeza. Mafunzo haya yamelenga kuhakikisha kuwa wajumbe wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe wanakuwa na uelewa wa kina wa mfumo wa NeST, hivyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ununuzi chuoni.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None