News-Details

News >Details

MZUMBE NA SUZA ZABADILISHANA UZOEFU KUBORESHA HUDUMA ZA MAKTABA

MZUMBE NA SUZA ZABADILISHANA UZOEFU KUBORESHA HUDUMA ZA MAKTABA

Chuo Kikuu Mzumbe kimepokea ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za uendeshaji na utoaji wa huduma za maktaba, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na kuboresha huduma za kitaaluma. Ziara hiyo imefanyika tarehe 1 Septemba 2026 katika Maktaba ya Chuo Kikuu Mzumbe, ambapo ugeni kitoka SUZA ulipata fursa ya kujifunza mifumo, taratibu na mbinu zinazotumika katika usimamizi na uendeshaji wa huduma za maktaba. Ugeni huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba wa SUZA, Dkt. Shehe Abdalla Mohammed akiambatana na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Watumiaji, Bi. Mwanakheir Abdalla pamoja na Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Kielektroniki, Bw. Haji Muhajir Ugeni huo ulipokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Kardo Mwilongo pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali vya Kurugenzi ya Maktaba. Katika ziara hiyo, wageni walielezwa kuhusu mifumo ya uendeshaji wa idara na vitengo, utoaji wa huduma kwa watumiaji, pamoja na matumizi, usimamizi na upatikanaji wa rasilimali za kielektroniki. Aidha, ziara hiyo ilitoa fursa kwa pande zote mbili kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu bora za kuongeza ufanisi wa huduma za maktaba, ikiwemo namna ya kukidhi mahitaji yanayobadilika ya wanafunzi, wahadhiri na watafiti katika mazingira ya elimu ya juu yanayoendelea kubadilika kiteknolojia. Ziara hiyo inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu, pamoja na kuendeleza mbinu bora za huduma za maktaba. Ushirikiano huo unatarajiwa kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa taarifa na rasilimali za kitaaluma na kuongeza ubora wa huduma kwa wanafunzi, wahadhiri, watafiti na jamii kwa ujumla.

None
None
None
None
None
None
None
None
None