News-Details

News >Details

WATUMISHI WAPYA WAPIGWA MSASA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA

WATUMISHI WAPYA WAPIGWA MSASA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA

Chuo Kikuu Mzumbe kimetoa mafunzo elekezi kwa watumishi wake wapya, wakiwemo wale waliopata ajira mpya na waliokaribishwa kupitia uhamisho kutoka taasisi nyingine, ili kuwajengea uelewa kuhusu taratibu za utumishi wa umma na matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA inayotumika Serikalini. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha TEHAMA wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Mohamed Ghasia, aliwasisitiza washiriki umuhimu wa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi wa chuo na taasisi kwa ujumla. "Ninawasihi mtumie maarifa mtakayopata hapa kwa ufanisi mkubwa. TEHAMA si tu nyenzo ya kurahisisha kazi, bali pia ni njia ya kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na usalama wa taarifa za taasisi. Ni wajibu wenu kuhakikisha mnasimamia mifumo hii kwa uadilifu na weledi mkubwa," alisema Dkt. Ghasia. Naye Mkuu wa Idara ya TEHAMA katika Huduma za Kiufundi na Matengenezo, Bw. Charles Kaijage, aliwakaribisha rasmi watumishi hao wapya na kuwataka kuwa tayari kujifunza na kushirikiana na wenzao katika kuhakikisha TEHAMA inatumika kwa ufanisi ndani ya chuo. Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa Kitengo cha TEHAMA, Bw. Mohamed Hanga, alibainisha kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha utendaji wa watumishi kwa kuwapa uelewa wa mifumo rasmi ya Serikali na taratibu za utumishi ndani ya taasisi. Mwezeshaji wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Afisa TEHAMA Mwandamizi, Bw. Alexander Benedict, aliwaelekeza washiriki kuhusu matumizi ya mifumo mbalimbali ya Serikali inayotumika katika taasisi za umma, ikiwa ni pamoja na PEPMIS, e-office, Government Mail na zinginezo. Bw. Benedict alisisitiza kuwa mifumo hii ni muhimu kwa kuhakikisha utendaji kazi wa umma unakuwa wa kisasa, wenye uwazi, na ufanisi mkubwa. Mafunzo haya yaliandaliwa na Kitengo cha TEHAMA Chuo Kikuu Mzumbe kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wake wapya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuendana na mabadiliko ya kidigitali ndani ya sekta ya umma.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None