News-Details

News >Details

MZUMBE KAMPASI YA TANGA: CHACHU YA MAPINDUZI YA ELIMU, AFYA NA UCHUMI MKINGA

MZUMBE KAMPASI YA TANGA: CHACHU YA MAPINDUZI YA ELIMU, AFYA NA UCHUMI MKINGA

Uwekezaji mkubwa unaotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe kupitia ujenzi wa Kampasi ya Tanga wilayani Mkinga unatarajiwa kuwa kichocheo muhimu cha mageuzi ya kielimu, kijamii na kiuchumi katika eneo hilo, huku ukifungua fursa mpya za elimu ya juu, huduma za afya, ajira, biashara na uwekezaji kwa wananchi wa Mkinga na maeneo jirani. Hayo yamebainishwa Septemba 12, 2026, wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kampasi hiyo iliyopo Kata ya Gombero, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga. Ziara hiyo iliyolenga kujionea hatua iliyofikiwa katika uwekezaji huo pamoja na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha miundombinu iliyosalia. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Shein ameueleza uwekezaji huo ni maono ya muda mrefu wenye manufaa mapana kwa jamii, akibainisha kuwa ubora wa majengo na miundombinu unaoonekana katika eneo hilo unaonesha dhamira na mipango endelevu ya kuhudumia vizazi mbalimbali. “Tunachokijenga hapa si kwa ajili yetu tu. Watakaokuja kunufaika zaidi ni watoto wetu, wajukuu zetu na vizazi vinavyofuata,” amesema Dkt. Shein. Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amebainisha kuwa Kampasi hiyo mbioni kuanza kutoa huduma, huku kazi kubwa iliyosalia ikiwa ni ukamilishaji wa maeneo mbalimbali ambayo mkandarasi anaendelea nayo kabla ya kuwa tayari kwa matumizi ya Kampasi hiyo na kuanza kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma zilizokusudiwa. Akizungumzia fursa zinazotokana na uwekezaji huo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Balozi Modest Jonathan Mero ameeleza kuwa uwepo wa Kampasi hiyo Mkinga ni fursa mpya ya maendeleo kwa jamii, hususani katika nyanja ya elimu, afya, biashara na uwekezaji, kutokana na mwingiliano wa kitamaduni kati ya wanafunzi, wataalamu na jamii. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na wadau wengine kuhakikisha changamoto zinazoweza kuchelewesha matumizi ya Kampasi hiyo zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati. Aidha, ametambua mchango wa viongozi wa vijiji waliowezesha upatikanaji wa eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 300 kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi hiyo, akieleza kuwa upatikanaji wa eneo hilo umeweka msingi muhimu wa utekelezaji wa uwekezaji huo mkubwa. Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, Karibu Kampasi ya Tanga – Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None