News-Details

News >Details

WAHADHIRI WA SKULI YA BIASHARA CHUO KIKUU MZUMBE WATOA ELIMU YA FURSA ZA MASOMO KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI

WAHADHIRI WA SKULI YA BIASHARA CHUO KIKUU MZUMBE WATOA ELIMU YA FURSA ZA MASOMO KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI

Wahadhiri kutoka Skuli ya Biashara ya Chuo Kikuu Mzumbe wamefanya ziara maalumu katika Shule za Sekondari Morogoro na Kola Hill kwa lengo la kuwaelimisha wanafunzi kuhusu fursa za masomo zinazotolewa chuoni hapo, hususan katika kozi za Ujasiriamali na Masoko. Wahadhiri hao walitoa elimu kuhusu umuhimu wa elimu ya biashara katika kujenga mustakabali bora wa wanafunzi, hasa katika dunia ya sasa inayotegemea ujuzi wa kibiashara na ubunifu wa kijasiriamali. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Munguatosha Mmbando alieleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinajivunia kuwa na programu zinazotoa ujuzi wa kina kwa wanafunzi, zikiwemo kozi za Ujasiriamali na Masoko, ambazo zinawaandaa wahitimu kuwa na uwezo wa kujiajiri na kushindana katika soko la ajira. "Elimu ya biashara si tu kwa ajili ya kuajiriwa, bali inatoa nafasi kwa wanafunzi kuwa wabunifu, kuanzisha biashara zao wenyewe, na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla," alisema Bw. Mmbando. Kwa upande wake, Bw. Lwako Lubida aliwataka wanafunzi wa shule hizo kufikiria kwa mapana zaidi kuhusu mustakabali wao wa elimu, akisisitiza kuwa Skuli ya Biashara ya Chuo Kikuu Mzumbe inatoa fursa adhimu kwa vijana wanaotaka kuwa sehemu ya mabadiliko katika sekta ya biashara hususan ujasiriamali na masoko. "Tuna programu mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya soko la sasa, hivyo tunawakaribisha wanafunzi wenye malengo na ndoto za kufanikisha maisha yao kupitia taaluma za biashara," alisisitiza Bw. Lubida. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi endelevu za Chuo Kikuu Mzumbe katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wa sekondari wanapata taarifa kuhusu fursa za elimu ya juu na umuhimu wa kujiandaa mapema kwa ajili ya safari yao ya kitaaluma.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None