News-Details

News >Details

BW. JUMA ZUBERI HOMERA AFANIKIWA KUTETEA TASNIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

BW. JUMA ZUBERI HOMERA AFANIKIWA KUTETEA TASNIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu, Bw. Juma Zuberi Homera, ameandika historia muhimu katika safari yake ya kitaaluma baada ya kutetea kwa mafanikio tasnifu yake ya Uzamivu (PhD), Utetezi wa tasnifu hiyo umefanyika leo tarehe 17 Machi 2025, Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro. Bw. Homera amefanya utetezi tasnia yake hiyo, mbele ya jopo la watahini wa tasnifu lililoongozwa na Prof. Frank Theobald uliojikita kwenye “ufanisi wa mabaraza ya ardhi ya vijiji katika kutatua matatizo ya matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.” Ulihusisha mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ameitaja kuwa ni Morogoro, Mbeya na Ruvuma. Akizungumza katika utetezi wa tafiti hiyo Bw. Zuberi alisema kutokuwa na elimu ya kutosha kwa wajumbe wa baraza ardhi ni moja ya sababu inayofanya washindwe kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi. Pia amesema kutokuwa na uwiano mzuri wa uwakilishi wa wakulima na wafugaji kwenye mabaraza hayo imekuwa sababu ya mabaraza hayo kufanya maamuzi yake kwa upendeleo. “Mabaraza ya ardhi hayana ufanisi mzuri katika kutatua matatizo ya matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji” alisisiza Bw. Homera Aidha akihitimisha utetezi wa utafiti huo Bw. Zuberi alitoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ili kuwezesha mabaraza ya ardhi ya vijiji kufanya kazi yake kwa ufanisi na kutoa mapendekezo kwa serikali kujenga uwezo wa kutosha wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa na hatimaye kuleta tija kwa taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Mwenyekiti wa jopo la watahini Prof. Frank Theobald baada ya mjadala wa kina, alitangaza kuwa Bw. Juma Zuberi Homera amefanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha kutetea tasnifu yake, na kuongeza kuwa huo ni ushindi mkubwa kwa Bw. Juma Zuberi.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None