News-Details

News >Details

WANAWAKE WAHAMASISHWA KUVISHINDA VIKWAZO KATIKA MASUALA YA UONGOZI NA UTAFITI

WANAWAKE WAHAMASISHWA KUVISHINDA VIKWAZO KATIKA MASUALA YA UONGOZI NA UTAFITI

Haya yalisemwa tarehe 18 machi kwenye warsha iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro, ambapo wanawake kutoka sekta mbalimbali walikusanyika kwa lengo moja: kuvishinda vikwazo vinavyowazuia kufanikiwa katika masuala ya uongozi na utafiti. Warsha yenye kaulimbiu “Kuvunja Vikwazo: Kuchochea Hatua kwa Wanawake katika Masuala ya Uongozi na Utafiti” iliwaleta wanawake pamoja kujadili changamoto wanazokutana nazo na mikakati ya kuzishinda katika nyanja hizo. Ilikuwa ni siku ya kuhamasisha na kuwajengea wanawake nguvu na matumaini, huku wakionesha uthubutu na mapenzi ya kweli ya kufanya mabadiliko katika jamii na kukuza nafasi zao katika utafiti na uongozi. Akifungua rasmi warsha hiyo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Eliza Mwakasangula, alieleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wanawake wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi na kushiriki katika tafiti mbalimbali. "Ni muhimu kuona wanawake wengi zaidi wakiongoza na kushiriki katika tafiti kubwa zinazochangia maendeleo ya nchi," alisema Prof. Mwakasangula huku akilipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa jitihada zake za kuwapa wanawake nafasi katika maeneo mbalimbali ya uongozi na kitaaluma. Awali, Prof. Elizabeth Lulu Genda, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo, alisisitiza umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kitaaluma na kijamii. "Tunapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi sawa za kushiriki katika utafiti na uongozi, bila kubaguliwa kwa misingi ya kijinsia," alisema Prof. Genda. Katika mjadala wa warsha, washiriki walibainisha changamoto kadhaa zinazowakwamisha wanawake katika uongozi na utafiti, ikiwa ni pamoja na mazingira yasiyo rafiki kazini, majukumu ya kifamilia, mitazamo potofu ya kijamii, na ukosefu wa mitandao ya usaidizi. Mhadhiri Mwandamizi kutoka Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti, Dkt. Anosisye Kesale, ambaye alikuwa Msemaji Maalumu katika warsha hiyo, alieleza kuwa kumwezesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None