News-Details

News >Details

CHUO KIKUU MZUMBE CHAWAFIKIA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUELEZA FURSA ZA ELIMU

CHUO KIKUU MZUMBE CHAWAFIKIA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUELEZA FURSA ZA ELIMU

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Kitengo cha Udahili pamoja na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kimetembelea Shule ya Sekondari Bwawani iliyopo Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani, na Shule ya Sekondari Sokoine Memorial iliyopo Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro. Ziara hii imelenga kuwaelimisha wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali za elimu zinazopatikana chuoni hapo. Katika ziara hiyo, wanafunzi wa kidato cha sita walipata nafasi ya kufahamu kwa kina kuhusu programu zinazotolewa katika ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada za Awali na Shahada za Umahiri. Vilevile, walielimishwa kuhusu tafiti zinazofanywa na chuo, huduma za ushauri wa kitaaluma, na mchango wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa jamii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Timu ya Chuo Kikuu Mzumbe ilieleza kuwa chuo kina miundombinu bora ya kujifunzia, wahadhiri wenye weledi, na mazingira mazuri ya kitaaluma yanayowajengea wanafunzi maarifa na ujuzi wa ushindani katika soko la ajira. Wanafunzi walionyesha shauku kubwa kwa kuuliza maswali kuhusu taratibu za udahili na sifa za kujiunga na chuo. Shauku yao ilijibiwa kwa kina, ambapo walipewa maelezo sahihi kuhusu hatua za kuomba udahili, vigezo vinavyohitajika kwa kila programu, pamoja na mwelekeo wa fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia katika safari yao ya elimu ya juu. Hii iliwawezesha kuwa na uelewa mpana wa jinsi wanavyoweza kufanikisha malengo yao ya kitaaluma katika Chuo Kikuu Mzumbe. Ziara hii ni sehemu ya mpango endelevu wa Chuo Kikuu Mzumbe wa kutembelea shule mbalimbali nchini kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kidato cha sita kufanya maamuzi sahihi ya kitaaluma na kufahamu fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo yao ya baadaye.

None
None
None
None
None
None
None
None
None