News-Details

News >Details

MZUMBE NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MBIONI KUANZISHA USHIRIKIANO WA KITAALUMA ILI KUONGEZA WIGO WA ELIMU YA URAIA NA KATIBA

MZUMBE NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MBIONI KUANZISHA USHIRIKIANO WA KITAALUMA ILI KUONGEZA WIGO WA ELIMU YA URAIA NA KATIBA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha ameongoza ujumbe wa Chuo ukijumuisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Hawa Tundui, Mtiva wa Kitivo Cha Sheria, Dkt. Sarafina Bakta, Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora, Dkt. Lawrencia D. Mushi na Mkurugenzi wa Shahada za Awali, Dkt. Orest Masue. Ujumbe huu umekutana na kufanya mazungumzo na Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Ndg. Eliakim Maswi. Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 16 Aprili 2025, Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Hii ni hatua ya awali za kuwezesha kuingia makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara na Chuo Kikuu Mzumbe ili kuweza kuja na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika kuhakikisha maudhui ya Elimu ya Urai na Katiba yanawafikia wanafunzi hasa kwa kuona namna ambavyo Mitaala ya Vyuo inaweza kuhuishwa kwa kuongeza maudhui husika. Katibu Mkuu Maswi amesema kuwa Wizara kupitia Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki imeanza maandalizi katika ngazi za Msingi na Sekondari na imeona ipo haja ya kuhakikisha inamjenga mtanzania kwa kumpatia maarifa ya kizalendo katika ngazi zote za elimu ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameipongeza Wizara kwa maono hayo ambayo yameanzia katika ngazi za chini za elimu na amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwani itawasaidia Watanzania kutambua tunu zao na kuziishi. Prof. Mwegoha ameweka bayana Chuo Kikuu Mzumbe kipo tayari kushirikiana na Wizara katika kutoa utaalamu kuhusu namna bora ya kukuza maono hayo. Aidha ameongeza kuwa ushirikiano huo unaweza pia kuhusisha uaandaaji wa pamoja wa mihadhara ya umma, kozi fupi na mahudhui mtandao yatakayosaidia kufikia lengo mahsusi la wizara na Chuo. Awali kikao hicho kilitanguliwa na taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Bi. Jane Lyimo ikielezea hatua mbalimbali zilizofanywa na Wizara katika kuwezesha Elimu hiyo inachopekwa katika ngazi mbalimbali za Elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya awali.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None