News-Details

News >Details

IDARA YA SAYANSI ZA JAMII NA INSIA YATOA SEMINA YA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU KWA WANAFUNZI WA SHAHADA YA AWALI YA RASILIMALI WATU

IDARA YA SAYANSI ZA JAMII NA INSIA YATOA SEMINA YA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU KWA WANAFUNZI WA SHAHADA YA AWALI YA RASILIMALI WATU

Katika kusimamia misingi ya utoaji wa elimu bora, wanataaluma kutoka Idara ya Sayansi za Jamii na Insia ya Ndaki ya Mbeya wameanda na kuendesha semina ya siku moja kwa wanafunzi wa Shahada ya Awali ya Rasilimali Watu(BHRM). Semina hiyo ilifanyika Tarehe 24 April, 2025 katika ukumbi wa Nkurumah Ndaki ya Mbeya. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkuu wa Idara ya Sayansi Jamii na Insia, Bw. John Jorojik ameeleza lengo la semina hiyo ni kukumbusha wanafunzi kuzingatia nidhamu, kuwajengea uwezo na kutambua wajibu wao kama wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe. “Semina hi ni muhimu kwenu kwa sababu inatoa fursa ya nyinyi kusahihisha pale mlipokosea na pia kuwakumbusha mambo muhimu na ya msingi ya kuzingatia ukiwa mwanafunzi wetu”. Juhudi hizi za wanataaluma zafuatia malengo ya Chuo Kikuu Mzumbe ya kuhakikisha wanafunzi hawapati elimu ya darasani pekee bali pia wanapata elimu maarifa ya kuchochea kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu na kujitambua ili wawe bora na wenye manufaa kwa chuo na jamii inayowazunguka. Katika semina hiyo, Wanataaluma walipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kuwa na ujuzi katika nyanja mbalimbali ili kuweza kutatua changamoto katika maisha yao na haswa kipindi ambacho bado ni wanafunzi. Pia, wanafunzi walikumbushwa kuhusu kuwa na bidii katika masomo. “Ukiwa kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu basi huna budi kuwa na ujuzi ambao utakusaidia katika mambo mbalimbali, mfano inabidi ujue namna ya kuwasiliana na watu vizuri, aina ya mavazi ya sehemu husika, itakusaidia sana katika safari yako ya mafanikio”. Bi. Yulither Nyanda, Mhadhiri Msaidizi. “Hapa chuo mmekuja kusoma na kufaulu ndio lengo namba moja kwenu, tafadhali ongezeni bidii ili muweze kufaulu vizuri. Mtaani mtu atakwambia kwani GPA kubwa kitu gani, mimi ninakwambia pata hiyo GPA kubwa uone faida yake. Jitambue unataka nini na uweke bidii usiondoke hapa na ufaulu mdogo huko nje ushindani ni mkubwa”. Alisema Bi. Maria Malamsha, Mhadhiri Msaidizi.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None