News-Details

News >Details

MZUMBE YAKUTANISHA WADAU KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA MIRADI YA MAENDELEO VIJIJINI UKANDA WA KILIMO KUSINI MWA AFRIKA

MZUMBE YAKUTANISHA WADAU KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA MIRADI YA MAENDELEO VIJIJINI UKANDA WA KILIMO KUSINI MWA AFRIKA

Chuo Kikuu Mzumbe kimeratibu na kuwakutanisha Wadau katika warsha ya kujadili matokeo ya utafiti wa miradi ya maendeleo vijijini na mabadiliko ya kiikolojia ‘Collaborative Researches Centers – CRC for Future Rural Afrika’ unaofadhiliwa na Baraza la utafiti la Ujerumani na kutekelezwa kwa pamoja kati ya vyuo vikuu vya Born na Kolon vya nchini Ujerumani pamoja na vyuo vikuu kutoka nchi za Kenya, Namibia , Zambia na Tanzania ikiwakilishwa na Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) . Akizungumza kwenye warsha hiyo iliyofanyika tarehe 25 April 2025 katika hoteli ya Morena jijini Dodoma, mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt.Nsubili Isaga amesema kuwa warsha hiyo imelenga kutoa matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa ushirikiano kati ya ‘CRC – Future rural Africa,’ Taasis ya Maendeleo endelevu ya nchini Ujerumani ( IDOS) na Watafiti kutoka nchi za Africa kwenye masuala ya migogoro ya ardhi, wakulima wadogo na uboreshaji wa miundombinu ya kisasa nchini Afrika ambayo imesisimua maendeleo kama vile mradi wa SGR Tanzania Kwa upande wake Prof. Anna Katharina Hornidge, Mkurugenzi wa IDOS nchini Ujerumani amesema kuwa utafiti huo umeweza kuonesha maarifa waliyonayo wakulima wadogo wanaoutumia njia za asili yakiunganishwa na mifumo ya kisayansi yataleta mapinduzi makubwa kwenye ukanda wa kilimo wa kusini. Ameongeza kuwa utafiti huo umewaunganisha Watafiti wanaoibukia walioko vyuoni na watafiti wakongwe na hivyo kwa pamoja wameweza kuleta matokeo ambayo yanaweza kuibadilisha Afrika kwenye nyanja ya maendeleo na kusisistiza kuwa Chuo kikuu Mzumbe kimekuwa ni Mshirika muhimu sana kwa kushirikiana na vyuo vingine katika nchi zinazoshiriki utafiti huo Awali Mratibu Mkuu wa mradi huo nchini Tanzania kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.Theobald Theodory amesema mradi huo ulianza mwaka 2018 na matokeo yanayowasilishwa ni ya awamu ya pili ya utafiti uliojikita kwenye maeneo ya ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji, migogoro ya Wakulima na Wafugaji pamoja na Sayansi ya Kilimo na kwamba uwasilishaji huo umewakutanisha Wadau wote muhimu kwenye sekta zilizoguswa na utafiti huo zikiwemo elimu,kilimo na maji ili kuisaidia Serikali kuweza kuandaa sera zitakazoleta utatuzi wa changamoto zilizobainika kwenye tafiti hizo . Ameongeza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimepewa heshima ya kuratibu warsha hiyo kubwa na muhimu kwa maendeleo ya nchi za Africa zinazoshiriki kwenye utafiti huo kwa kuwa kilishiriki kwenye hatua za awali za kubuni na kuandika mradi huo na kimeshafanya tafiti nyingi na kuandaa machapisho mengi ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwenye mradi huo. Katika hatua nyingine Mwanafunzi anayesomea mifumo ya kiteknolojia chuo Kikuu Mzumbe Bi. Anna Robert, ameeleza namna matokeo ya tafiti hizo yalivyomfungulia fursa ya kubuni mifumo ya kiteknolojia itakayowasaidia Wakulima wadogo kurahisisha na kuboresha utendaji wa shughuli zao za kilimo pamoja na mifumo itakayosaidia kupunguza migogoro ya ardhi na hivyo kusaidia kuleta maendeleo kwa Wanajamii wa vijijini

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None