News-Details

News >Details

WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU MZUMBE NDAKI YA DAR ES SALAAM WAFANYA BONANZA KUIMARISHA UTENDAJI NA USHIRIKIANO KAZINI

WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU MZUMBE NDAKI YA DAR ES SALAAM WAFANYA BONANZA KUIMARISHA UTENDAJI NA USHIRIKIANO KAZINI

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam wameshiriki bonanza maalum la michezo lililofanyika katika Fukwe za Empire, Bagamoyo, Mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mshikamano, afya na mahusiano bora kazini kwa ajili ya kuongeza tija katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku. Bonanza hilo ambalo limefanyika katika siku ya kumbukizi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, liliwaleta pamoja wafanyakazi wa Idara mbalimbali wakiwemo wahadhiri, watendaji wa utawala, ambapo wameshiriki michezo mbalimbali ya kufurahisha na kuchangamsha akili kama mpira wa wavu na ufukweni, draft, bao, karata na michezo ya ubunifu. Akizungumza leo April 26, 2025 Mkoani Pwani, wakati wa Bonanza hilo, Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Biashara, Dkt. Joshua Mwakujonga, amebainisha kuwa bonanza hilo limekuwa na faida kubwa kwa wafanyakazi kwa kuwa limesaidia kubomoa matabaka kazini na kujenga mahusiano ya karibu baina ya wafanyakazi wa kada mbalimbali. Kwa upande wake, Afisa Tawala wa Idara ya Huduma za Kitawala Bi. Clara Paschal Kille, amesema kuwa bonanza hilo limechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza afya za wafanyakazi kupitia michezo mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa michezo ya akili kama draft, bao na karata katika kuimarisha uwezo wa kufikiri na kupunguza msongo wa mawazo. Bi. Kille ametoa wito kwa wafanyakazi wote wa Ndaki hiyo kuhakikisha wanajitokeza kuchangamkia fursa ya kushiriki bonana kwani ni muhimu kwao. Naye Naibu Mshauri wa Wanafunzi wa Ndaki hiyo, Bi. Zitta Victoria Mnyanyi, amesema kuwa kila mwaka chuo hutenga siku maalum kwa ajili ya wafanyakazi kukutana, kuburudika na kujifunza kutoka kwa wenzao katika mazingira tofauti na eneo la kazi. Amesisitiza umuhimu wa kushiriki michezo ili kuwa afya njema, mshikamano na maelewano kwani ni msingi wa utendaji kazi wenye mafanikio kwa Taifa. Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa taasisi bora za elimu ya juu nchini, na kujivunia kutoa elimu bora yenye kulenga maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa mujibu wa kauli mbiu yao "Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu."

None
None
None
None
None
None
None
None
None