News-Details

News >Details

BW. MWANDU JIYENZE ATETEA VYEMA TASINIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

BW. MWANDU JIYENZE ATETEA VYEMA TASINIFU YAKE YA UZAMIVU CHUO KIKUU MZUMBE

Katika hatua muhimu ya safari yake ya kitaaluma, Bw. Mwandu Jiyenze, mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Kitivo cha Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu Mzumbe, amefanikiwa kutetea tasnifu yake kwa mafanikio makubwa. Utetezi huo umefanyika leo, 17 Machi 2025, katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro, mbele ya jopo la watahini lililoongozwa na Prof. Ernest Kihanga. Utafiti wake umeangazia mipango ya kimkakati na athari zake katika utoaji wa huduma za afya kwenye halmashauri nchini Tanzania. Akiwasilisha matokeo ya tafiti hiyo, Bw. Jiyenze alieleza kuwa uhaba wa rasilimali, changamoto za usimamizi, na ukosefu wa ufuatiliaji wa karibu wa sera za afya ni miongoni mwa mambo yanayokwamisha utekelezaji wa mipango hiyo. "Ili mipango ya kimkakati iwe na matokeo chanya, ni lazima kuwe na usimamizi makini na rasilimali za kutosha kwa utekelezaji wake," Alisisitiza Bw. Jinyenze wakati wa utetezi wake. Katika mapendekezo yake, alieleza kuwa kuimarisha usimamizi wa rasilimali, kushirikisha jamii katika upangaji wa mikakati ya afya, na kuhakikisha sera zinakidhi mahitaji ya wananchi ni hatua muhimu zitakazosaidia kuboresha sekta ya afya katika ngazi ya halmashauri. Baada ya mjadala wa kina, Mwenyekiti wa jopo la watahini, Prof. Ernest Kihanga, alitangaza kuwa Bw. Jiyenze ametetea tasnifu yake kwa ufanisi mkubwa, huku akibainisha kuwa matokeo ya utafiti wake yana mchango muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini. Hatua hii inaendelea kuthibitisha nafasi ya Chuo Kikuu Mzumbe kama nguzo muhimu ya tafiti zenye tija kwa maendeleo ya jamii na sekta mbalimbali nchini. Chuo Kikuu Mzumbe, Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu

None
None
None
None
None
None
None
None
None