News-Details

News >Details

UKAGUZI WA MAENDELEO YA UJENZI WA KAMPASI MPYA YA CHUO KIKUU MZUMBE – TANGA WAFANYIKA

UKAGUZI WA MAENDELEO YA UJENZI WA KAMPASI MPYA YA CHUO KIKUU MZUMBE – TANGA WAFANYIKA

Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Eliza Mwakasangula, akiambatana na waratibu wengine wa mradi, amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe katika eneo la Kata ya Gombero, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga Machi 24, 2025. Ziara hiyo imelenga kufuatilia hatua za utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya elimu ya juu nchini. Akizungumza wakati wa ukaguzi, Prof. Mwakasangula ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kampasi hiyo, akieleza kuwa maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa ni ya kuridhisha. Ametoa pongezi kwa Mkandarasi mzawa wa Dimetoclasa Real Hope Limited pamoja na Mshauri Elekezi, kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kushirikiana kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa viwango vya juu. "Mradi huu ni wa kimkakati, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa ubora wa ujenzi unazingatiwa kuanzia hatua za awali hadi kukamilika kwake. Pia, natoa rai kwa mkandarasi kuimarisha mahusiano mazuri na jamii inayozunguka eneo la mradi, kwa kuwa wao ndio walinzi wakubwa wa miundombinu hii," amesema Prof. Mwakasangula. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, hadi Vijiji, akibainisha kuwa Serikali tayari imewekeza katika miundombinu muhimu kama barabara na umeme, ambazo zimefikishwa hadi eneo la ujenzi. Pamoja na hayo, Prof. Mwakasangula amemtaka mkandarasi kuzingatia kikamilifu sheria, taratibu, na kanuni za usalama mahala pa kazi, huku akihimiza kuendelea kulinda mazingira na kuzingatia hifadhi yake katika utekelezaji wa mradi huo. Kwa upande wake, Kaimu Msimamizi wa eneo la ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe - Tanga, Bw. Goodluck Sarikoki, kutoka kampuni ya Dimetoclasa Real Hope Limited, amepongeza ziara hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati uliopangwa.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None