News-Details

News >Details

BARAZA LA WAFANYAKAZI MZUMBE LAWASHA MOTO WA MAENDELEO YA CHUO

BARAZA LA WAFANYAKAZI MZUMBE LAWASHA MOTO WA MAENDELEO YA CHUO

Chuo Kikuu Mzumbe kimefanya Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Tano la Wafanyakazi uliolenga kuimarisha mazingira bora ya kazi na ustawi wa watumishi wa chuo hicho. Mkutano huo umefanyika leo Tarehe 29 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kuongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, akisaidiana na Katibu wa Baraza, Dkt. Lukiko Lukiko. Akifungua rasmi mkutano huo, Prof. Mwegoha amewasihi wajumbe kuwa mabalozi wazuri wa Chuo katika maeneo yao ya kazi kwa kutanguliza uzalendo, weledi, na uwajibikaji kwa kuwa kila mtumishi ana mchango muhimu katika kuyafikia malengo ya pamoja ya taasisi. “Tunahitaji mshikamano wa dhati kama familia ya Mzumbe. Baraza hili lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi na kwa maslahi ya taasisi. Sote ni sehemu ya chapa ya Chuo Kikuu Mzumbe – tuendelee kuilinda, kuithamini, na kuikuza,” alisisitiza Prof. Mwegoha. Aidha, alieleza kuwa mafanikio ya taasisi hayawezi kupatikana bila mshikamano wa kweli kati ya viongozi na watumishi wa ngazi zote hivyo aliwataka wajumbe kuwa na mtazamo chanya, bidii ya kazi, na moyo wa kujitolea ili kutimiza malengo makuu ya taasisi. Vilevile, Prof. Mwegoha alihimiza ushiriki wa watumishi wote katika shughuli za kijamii na kitaifa, hasa katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), akifafanua kuwa siku hiyo ni fursa ya kuonesha mshikamano, kujifunza, na kusherehekea mafanikio ya pamoja. Kwa upande wake, Katibu wa Baraza, Dkt. Lukiko Lukiko, alisisitiza nafasi ya Baraza hilo katika kuimarisha utendaji kazi na kuchochea uwajibikaji miongoni mwa wajumbe ili kuhakikisha kuwa maamuzi yanayochukuliwa yanakuwa na manufaa kwa Chuo na watumishi wake. Mkutano huo ulihitimishwa huku wajumbe wakionesha ari, mshikamano, na dhamira ya dhati ya kuendelea kushirikiana katika kuleta maendeleo chanya kwa Chuo Kikuu Mzumbe.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None