News-Details

News >Details

KARAMU YA JIONI ILIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU MZUMBE KWA WASHIRIKA YAFANA

KARAMU YA JIONI ILIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU MZUMBE KWA WASHIRIKA YAFANA

Katika kusherehekea siku ya Chuo Kikuu Mzumbe na Kambi ya wajasiriamali ya chuo hicho iliyopamwa na mambo mbalimbali ikiwemo hafla ya chakula jioni iliyojumuisha wafanyakazi, wadau mbalimbali wa chuo hicho wakiwemo wajasiriamali waliosoma na wanaosoma chuoni hapa imefanyika tarehe 7 Mei 2025 Kampasi Kuu Morogoro. Akifungua hafla hiyo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Hawa Tundui aliwapongeza kamati ya maandalizi kwa kuandaa hafla hiyo kwa ufanisi mkubwa “tunawashukuru sana kutakutanisha wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Mzumbe ili tujuane na tufurahi pamoja lakini pia nawapongeza kwa kuweza kuwakusanya wadau mbalimbali wa chuo hiki na kuwaleta pamoja.”alisema Prof. Tundui Katika halfa hiyo mjadala kuhusu changamoto na mikakati ya utekelezaji wa makubaliano ya maelewano (Memorandum of Understanding) ulifanyanyika na kuainisha changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Makubaliano ya maelewano ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha, watu na vifaa pamoja na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa ufuatiliaji na Tathimini na kuainisha mikakati mbalimbali ya kuboresha utekelezaji wa Makubaliano ya maelewano. Aidha, baadhi ya wajasiriamali waliopata fursa ya kushiriki katika hafla hiyo walitambulisha bidhaa wanazozizalisha na kuziuza ambao wengi wao wakiwa ni wanafunzi wanaosoma chuoni hapa na wale waliohitimu miaka iliyopita ambapo walikishukuru na kukipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa ushirikiano unaowapatia katika kukuza na kuendeleza biashara zao hivyo kuendelea kujikwamua kiuchumi na kukiomba chuo hicho kuendeleza uhusiano huu kwa manufaa yao na ya wajasiriamali wengine wanaoendelea kuibukia kutoka chuoni hapo. Akizungumza wakati wa kufunga hafla hiyo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi aliwashukuru wote waliojumuika katika hafla hiyo na kusisitiza kwamba halfa hiyo ni mwendelezo wa kusaidia wafanyakazi kupata muda wa kujuana, kufahamiana na kufurahia pamoja pia aliwapongeza wajasiliamali wote waliojitokeza na kushiriki katika hafla hiyo na kuwashukuru wanajopo wote waliohusika kwenye majadiliano yaliyoleta ufahamu juu ya changamoto zinatokana na Makubaliano ya maelewano pamoja na mikakati mahususi ya kusaidia ufanisi wa makubaliano hayo. “Chuo kikuu Mzumbe, tujifunze kwa maendeleo ya watu”

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None