News-Details

News >Details

CHUO KIKUU MZUMBE KUTOA MWONGOZO WA MATUMIZI YA AKILI MNEMBA

CHUO KIKUU MZUMBE KUTOA MWONGOZO WA MATUMIZI YA AKILI MNEMBA

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma,Tafiti na ushauri Prof. Hawa Tundui amesema Chuo Kikuu Mzumbe kinaandaa mwongozo wa matumizi ya akili mnemba (Artificial Inteligence) kwa kuwa matumizi ya teknolojia hiyo hayakwepeki katika dunia ya sasa na kwamba yana umuhimu mkubwa kwa elimu ya juu ikiwa yatatumika vizuri kwenye shughuli za ufundishaji na ujifunzaji. Prof. Tundui ameyasema hayo Mei 14, 2025 wakati akifungua warsha ya mafunzo jumuishi kuhusu matumizi ya teknolojia kwa Wanataaluma wapya walioajiriwa na Chuo Kikuu Mzumbe. Mafunzo hayo yamewezeshwa na mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) na yanafanyika mjini Morogoro kwa siku tatu. “Sio haramu kutumia akili mnemba katika kujifunza na kufundishia isipokuwa ni namna ya kuitumia. Wizara ya Elimu wameandaa mwongozo na sisi Chuo Kikuu Mzumbe tutaandaa mwongozo wetu ili Wanataaluma waweze kuitumia akili mnemba kwa uhuru zaidi na ndiyo sababu tunawajengea uwezo Wanataaluma wapya wa jinsi ya kutumia teknolojia zote za ufundishaji .” Alisema Prof. Tundui Aidha Prof. Tundui ameongeza kuwa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa Wanataaluma ni mwanzo wa safari ya Chuo Kikuu Mzumbe kuanza kutoa elimu ya masafa (Blended Learning) katika mwaka mpya wa masomo utakaoanza Oktoba 2025, kwa kozi zilizoidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na kufafanua kuwa aina hiyo ya ufundishaji itamuwezesha Mwanafunzi kusoma 60% ya masomo yake kwa njia ya mtandao na kuhudhuria madarasa kwa wiki chache na nyakati za mitihani pekee katika kipindi chote cha masomo yake na itatoa fursa ya kujiendeleza kimasomo kwa Watu wengi wenye changamoto ya kukosa muda wa kuhudhuria madarasa Katika kipindi chote cha mafunzo Wanataaluma hao watajengewa uwezo juu ya uundaji na matumizi ya hifadhi data za Rasilimali za Elimu Huria (OER), mafunzo ya ujuzi laini (Soft skills) na uundaji wa maudhui ya kozi za mtandaoni, utengenezaji wa maktaba za kidijitali na matumizi ya akili mnemba.

None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None
None